Sambaza....

JUMLA ya mabondia 16 wanatarajia kupanda ulingoni katika mapambano nane ya utangulizi kuelekea katika pambano Seleman Kidunda dhidi ya Eric Mukadi linatarajia kupigwa Juni 30, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar.

Mbali ya Kidunda ambaye atacheza na Mukadi kutoka DR Congo lakini bondia Mfaume Mfaume atapanda ulingoni kwenye pambano hilo dhidi ya Mkululeko Mhlongo raia wa Afrika Kusini katika pambano la mwisho la utangulizi kabla ya Kidunda kupanda ulingoni kwenye pambano hilo ambalo limeandaliwa na Kampuni ya Promosheni ya ngumi za kulipwa nchini, Paf Promotion Company Limited.

Promota wa hilo kutoka PAF Promotion Company Limited, Fadhili Maogola alisema kuwa maandalizi ya pambano hilo yanaendelea vizuri ambapo watakuwa na jumla ya mapambano kumi yatakawakutanisha mabondia 20 wakiwemo watatu kutoka nje ya mipaka ya Tanzania.

Bondia wa ngumi za kulipwa Selemani Kidunda akimwaga wino na kuthibisha kuwepo katika pambano la June 30, Mlimani City.

“Kwanza tunashukuru Mungu maandalizi ya pambano letu la hata usipo lala pata kucha yanaendelea vizuri na matarajio yetu ni kuona tunaenda kuijaza Mlimani City kwa kushuhudia pambano kubwa ndani ya mwaka huu ambalo litajumuisha mabondia wengi wa kubwa.

“Ukiacha maandalizi ya mabondia lakini jambo kubwa kwa sasa juu ya mapambano yenye ambapo mapambano yote yatakuwa kumi yakiwa na jumla ya mabondia 20 lakini mapambano nane yatakuwa ya utangulizi ambayo yatakuwa na mabondia 16 kabla Mfaume Mfaume Mfaume ‘Mapafu ya Mbwa’ kukamilisha pambano la tisa la utangulizi na kisha Seleman Kidunda kufunga dimba na Mukadi, ” alisema Maogola.

Lakini kwa upande wa mapambano hayo ya utangulizi bondia Fadhili Majiha ‘Stopper’ atapanda ulingoni dhidi ya Jamal Kunoga wakati Saleh Kasim atamalizana na Said Bwanga kabla ya Deo Samweli kumvaa Adam Ngange.

Mfaume Mfaume atakuepo June 30 Mlimani City.

Wengine ni Pius Mpenda ambaye atapanda ulingoni dhidi ya Simon Tichecha wa Malawi wakati Rama Jonh Cina akitarajia kupasuana na Yona Segu lakini Omary Maulid atapanda na Shaban Kibiriti na Boniface Seguda atacheza na Hamza Mahamoudu huku Herry Rashid akitarajia kumalizana Hussein Pendeza.

Sambaza....