Sambaza....

Klabu ya Yanga saa sita kamili usiku ilimtambulisha mchezaji wao mpya baada ya usajili kufunguliwa rasmi July moja mwaka huu na kuwa mchezaji wakwanza wa Wananchi kutambulishwa usajili huu.

Yanga imemtangaza Nickson Kibabage alietokea Singida Fountaine Gate kama mchezaji wao mpya atakaekwenda kusaidiana na Joyce Lomalisa katika eneo la ulinzi wa kushoto. Kufutia usajili huo mwandishi wa habari Juma Ayo ametoa maoni yake baada ya usajili huo.

“Kwa Mtazamo wangu huu usajili wa Kibabage sio usajili mbaya ila kwangu ni mchezaji wa kawaida, ukiangalia kazi waliyofanya wachezaji kama akina Djuma Shabaan ambaye anatajwa anaweza kuondoka wakati wowote bado unaona Kibabage ana kazi kubwa ya kufanya,” alisema Ayo.

Nickson Kibabage.

Juma pia ameiambia Yanga haoni ni kwa jinsi gani Kibabage ataisaidia timu hiyo katika michuano ya kimataifa kwani uwezo wake wa ushindani ni mdogo bado.

“Katika Mtazamo wa kushindana kwenye michuano ya kimataifa Kibabage bado sana, amewahi kusajiliwa kwenye vilabu vikubwa vyenye ushindani na alishindwa kufanya vizuri.”

Achana na changamoto yake ya kimo katika eneo analocheza lakini tuangalie ufanyaji kazi  wake na wachezaji waliokuwa kwenye nafasi hiyo Yanga, acha tuendelee kuona nani ataachwa au kuongezwa lakini kwa maoni yangu Kibabage anaweza kuwa mchezaji mbadala lakini siyo mchezaji wa kutegemewa hasa kwa namna ambavyo tunaona dhamira ya Yanga msimu ujao kwenda kushindana kimataifa.”

Nickson Kibabage

Nae kocha na mchambuzi Tigana Lukinja amempongeza Kibabage kwa usajili huo lakini hakuonyesha kushangazwa na hatua za kijana huyo.

“Nimemfahamu akiwa’ kijivulana kidogo’ sana miaka kadhaa nyuma nikamtabiria makubwa kwa kipaji chake na mwenendo wake aliyouonesha tangu akiwa na umri huo. Achana na ‘mguu wake wa dhahabu’ ambao kwa mchezaji mpira anayetumia huo kufa masikini ni kuhitaji mwenyewe,” alitania Tigana na kuongeza

“Bwana ndogo huyu alijiandaa vyema akilini kwake kucheza mpira mkubwa ndiyo maana hata alivyopata nafasi ya kwenda Morocco Difaa el Jadida akiwa na umri ule sikushangaa chochote.

Ameunganisha vyema safari yake kwenye timu za Taifa toka vijana hadi yawakubwa na kwa sasa toka vilabu vya kawaida hadi timu kubwa.”

Sambaza....