Sambaza....

Wapwa:: Unafahamu kuwa wachezaji zaidi ya 75% duniani wanaamini katika’ kiatu cha bahati’.

Kwa wale waliocheza kwenye top level (professional) wengi wao wanamikataba na makampuni makubwa ya utengenzaji viatu au vifaa vya michezo kama vile

Adidas,Puma, Nike, Lotto, Asics, Umbro,
Joma nk hivyo ni kawaida ya mchezaji moja kuwa na viatu vingi anavyovitumia ndani ya msimu.

Hata hapa kwetu jambo hilo lipo sana ,wapo wachezaji wenye viatu pea 3 hadi 4 na zaidi japo nadhani wote hawana ‘endorsement’ hivyo wanachanganya makampuni.

Kiatu cha Sadala

Point yangu kila mchezaji mpira wenye uwezo wa kuwa na viatu vingi huwa anaamini kwenye kiatu chenye bahati kwake akikivaaa anapeform vizuri, mfano yupo anayeamini akivaa kiatu chake fulani miongoni mwa pea zake atafunga goli au atacheza vizuri.

Nadharia hii inathibitishwa pia na Michael Owen wakati wa ubora wake aliwahi kusema kuna moja ya pea ya viatu vyake akivaa lazima atupie

Michael Owen akiwa na kiatu

Niliwahi kupost kuhusiana na kiatu kilichokuwa kinavaliwa na Abeid Mziba ‘Tekero ‘ baadaye kilikuja kuwa maarufu sana nikasimulia kisa chake cha kutumia msimu mzima na kufunga magoli kadhaa lakini siku alivyokivaa kwenye mchezo wa fainal wa Taifa Cup yakati hizo ndiyo ikapata kuitwa rasmi hivyo

Abeid Mziba

Lakini aliniambia alikuwa na viatu vingine vingi ikiwemo Copa mundial ya ngozi ila alipokuwa anavaa ya Canvas alikuwa anafunga

Wewe binafsi unaamini upande upi? Kuna mahusiano ya kiatu na bahati ya kucheza vizuri ikiwemo kufunga au hakuna bahati?

Sambaza....