Beki wa kulia wa Timu ya taifa ya Tanzania “Taifa Stars” anayecheza soka la kulipwa nchini Zambia, Hassan Kessy na mshambuliaji wa timu ya taifa Thomas Ulimwengu anayecheza soka la kulipwa nchini Sudan wataikosa mechi ya marudiano dhidi ya Cape Verde itakayochezwa kesho Jumanne.
Wachezaji hao wote wawili wana kadi mbili za njano, kadi ambazo zitawasababisha wakose mchezo huo. Taifa Stars inahitaji ushindi katika mechi hiyo baada ya kufungwa goli 3-0 katika mchezo uliofanyika nchini Cape Verde. Katika kundi hili Uganda inaongoza ikiwa na alama 7 , Cape Verde inashika nafasi ya pili ikiwa na alama 4, Lesotho inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama 2 na Tanzania ikishika nafasi ya mwisho ikiwa imejikusanyia alama 2.