Sambaza....

Mwanasheria wa mwanadada Kathryn Mayorga, Leslie Stovall anatarajia kusafiri kuelekea jijini London kukutana na mpenzi wa zamani wa Mwanakandanda Cristiano Ronaldo, ambaye ni mwanamitindo na mwanahabari Jasmine Lennard.

Leslie ameamua kufunga safari hiyo baada ya Jasmine kusema kuwa ana taarifa muhimu kuhusu Cristiano Ronaldo, taarifa ambazo zinaweza kuwasaidia katika kesi yao waliyoifungua ya kubaka inayomuhusisha mwanakandanda huyo nguli duniani.

Lennard ambaye alikuwa mpenzi wa Ronaldo miaka 10 iliyopita ameoneka kwa siku kadhaa kumtupia maneno makali staa huyo kwenye mitandao yake ya kijamii na hata alionekana kwenye kipindi cha luninga cha Celebrity Big Brother aliendelea kumponda mwanakandanda huyo.

Leslie amesema maelezo ya mwanadada huyo yanaweza kuwasaidia katika kesi yao ya ubakaji, na kwamba kwa kuwa alikuwa mpenzi wake basi kuna uwezekano wa mambo mengi zaidi kuwekwa hadharani katika tukio hilo lilitokea katika hotel ya Las Vegas.

Wakati ambapo Ronaldo na wanasheria wake wakiendelea kupinga shutuma hizo, tayari polisi nchini Marekani waliagiza sampuli ya DNA ya mwanasoka huyo aliyewahi kuwika na timu za Manchester United na Real Madrid.

Sambaza....