Katika mechi 44 Tanzania ilizokutana na Kenya, Tanzania imeshinda mechi 14, sare 14 na kupoteza 20.
Mechi ya kwanza ilikuwa Septemba 4, 1964 na Tanzania ilishinda 1-0 dhidi ya Kenya katika Kombe la Afrika Mashariki (CECAFA sasa).
Mechi ya mwisho kabla ya leo Kenya ilishinda 1-0 katika michuano ya CECAFA.
Kenya imewahi kupata kipigo kikali cha 5-0 wakati wa kampeni za kutafuta nafasi ya kucheza kombe la dunia. Mechi ilichezwa 19 Julai 1980. Lakini tano hizo zilikuja kulipwa baadae katika mechi ya kirafiki.
Leo majirani hawa wanakutana karika michuano mikubwa ya Kombe la Mataifa ya Afrika kule nchini Misri ambako mto Nile ambao ni mkubwa na unaotegemewa kwa kilimo na matumizi chanzo chake ni Afrika Mashariki zinakotoka timu hizi.