Na Lilian Mukulu.
Wamukelekile Ekhaya Lami Formula 1…(Karibu nyumbani kwangu Formula 1)
Nimeamua kuandika kizulu kwani licha ya Formula 1 kuwa ni moja ya mchezo pendwa duniani, ukichezwa katika nchi mbali mbali ila kwa upande wa bara la Afrika mara mwisho kushuhudia mbio hizo ilikuwa miaka 29 iliyopita katika Circuit ya Kyalami.
Kyalami inapatikana Afrika kusini katikati ya majiji makubwa mawili yani Cape town na Pretoria. Kwa lugha ya Kizulu Kyalami inamaanisha nyumbani kwangu.
Circuit hii ilitengenezwa mwaka 1961 kipindi ambacho wazee wetu hapa nyumbani wakipambania Uhuru wa Tanganyika mahususi kabisa kwa ajili ya mbio za magari .
Novemba 4, 1961 kwa mara ya kwanza watu walishuhudia mbio za kwanza za magari Kyalami, circuit hii inaurefu wa kilometa 4,104 inakumbukwa sana kutokana na bara bara zilizonyooka.
John Love na Dawie Gous wakiendesha gari aina ya Porsche 550 Spyder waliibuka washindi wa mbio za kwanza za magari kufanyika Kyalami.
Katika miaka tofauti tofauti walishuhudia nyota mbali mbali wa langalanga kipindi kile wakifanya wakishindana kutafuta nani bingwa wa michuano ya dunia ya Formula 1 pale Kyalami na kilikuwa kivutio kikubwa sana pale.
Kila kizuri kinaupande wake wa maumivu moja la tukio baya kuwahi kutokea katika Circuit ya Kyalami ni kifo cha dereva wa Muingereza Tom Pryce na Marshal Fredirck Jansen baada ya gari la Renzo Zorzi kupata shida kidogo na Fedrick akiwa ameshika fire extinguishers waliingia kumsaidia Ila kwa bahati mbaya Tom alimgonga na kumrusha juu akaja kuangukia kwenye gari la Tom na kufa hapo huku Fire Extinguishers aliyoishika ilimpiga Tom kichwani na hapo ndipo umauti ulipompata.
Baada ya maeneo karibu ya Circuit kubadilishwa na kuwa makazi ya watu mwaka 2014 mfanyabiashara maarufu wa magari Toby Venter aliamua kupanunua kwa randi million 205 na 2015 marekebisho ya Kyalami yalianza, mfano kutengeneza barabara zitakazo kuwa zinatumika, sehemu ya mashabiki na hata sehemu za pit yani sehemu magari yatakapokuwa yafanyiwa marekebishi wakati mbio zinaendelea.
Bingwa mara saba wa Formulating one Lewis Hamilton Octoba 31 alishauri Formula 1 kufufua grandpix ya Afrika Kusini maana yake ni ufufuo wa Kyalami.
Mtendaji mkuu wa Grand Prix ya Afrika kusini Warren Scheckter anaamini kuanzia 2023 watakuwa tayari kuleta tena Formula 1 katika bara la Afrika baada ya miaka 29.