- Safari ya Yanga, Mikononi mwa Dube
- Simba na Yanga nani anaongoza kuweka mpira kwapani.
- Yanga Waweweseka! Gamondi Nje!
- Fadlu Tunaamini anawapa Ubingwa Wekundu
- Manuel Neuer ana umri sawa na uchambuzi wa soka kwa kompyuta
Baada ya Kocha wa timu ya Taifa, Emmnauel Amunike kuita kikosi chake na kumjumuisha kiraka majeruhi Shomari Kapombe, wadau wengi wa soka wanahoji kwanini Amunike amuite hali ya kuwa, bado ni marejuhi?
Katika kujibu swali hilo, kandanda.co.tz ilifanya juhudi kubwa kujua hali ya kapombe kwa sasa na kuona kama kutakuwa na uwezekano wa beki huyo kutumika katika timu ya taifa na hata Simba.
Kwa taarifa zilizopo ni kwamba, Shomari Kapombe amebadilishiwa kitengo cha matibabu, na sasa yupo chini ya wataalamu wa mazoezi ya viungo (physioTherapy).
Hayo yamethibitishwa na daktari wa timu ya Simba Yassin Gembe, ambaye ameeleza kuwa, Beki huyo wa shavu la kulia, hayuko chini yao, bali yuko na wataalamu wa mazoezi ya viungo, na wao wanasubiri taarifa rasmi ya wataalamu hao juu ya hali yake na ikiwezekana aanze kutumika katika mechi za Simba na timu ya taifa.
Hali ya kapombe inaonekana kuwa na mabadiliko makubwa chanya, kwa sasa ana wiki tatu tangu aanze kufanya mazoezi na wataalamu wa Gym, na inakadiliwa kuchukua muda mfupi zaidi kwa kapombe kuanza kufanya mazoezi na wenzake uwanjani.
Hivyo ni dalili kuwa, kapombe huenda asitumike katika mechi za Simba zilizosalia lakini anaweza kutumika na timu ya taifa, kwani kuna muda mrefu kabla ya mashindano ya AFCON kuanza mwezi Juni nchini Misri.
Mbali na Kapombe, akizungumzia hali ya Paschal Wawa, amesema kuwa, wawa anaendelea vizuri na ataungana na timu baada ya mechi dhidi ya Mbeya City ya Mkoani Mbeya