Sambaza....

Kiraka wa klabu ya Kagera Sugar Nasoro Kapama anatajwa kumalizana na “Wekundu wa Msimbazi” Simba hata kabla ya msimu kumalizika.

Mchezaji huyo wa zamani wa Ndanda Fc kwa sasa anaitumikia Kagera Sugar huku mkataba wake ukiwa unaelekea ukingoni, mkataba wake unaisha baada ya msimu huu kumalizika.

Nasoro Kapama akimiliki mpira mbele ya Lamine Moro.

Nasoro Kapama mwenye uwezo wa kucheza kama mshambuliaji namba 10, kiungo wa ulinzi na mlinzi wa kati inasemekana ni miongoni mwa mapendekezo ya kocha Selemani Matola.

Kutokana na akili kubwa ya mpira aliyokuwa nayo ndio  sababu kubwa inayomfanya aweze kucheza maeneo tofauti uwanjani na ndicho kilichoivutia zaidi Simba.

Sambaza....