Sambaza....

Kiungo wa Simba anayecheza eneo la kiungo cha kuzuia Jonas Mkude amepata majeraha katika mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC FC uliochezwa katika uwanja wa mazoezi wa Simba SC wa Mo-Simba Arena.

Kwenye mchezo huo ambao Simba walifanikiwa kupata ushindi wa goli 3 kwa 1 . Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye klabu hiyo iliyotolewa na daktari wa klabu hiyo , Dkt. Gembe amedai kuwa Jonas Mkude ameumia vidole vya miguu.

Maumivu haya ya vidole vya miguu vitamfanya akae nje kwa wiki mbili , ndani ya hizo wiki mbili atakosa michezo minne ambayo ni dhidi ya Ruvu Shooting , Mwadui FC , Tanzania Prisons na Mbeya City.

Dkt. Gembe ameuambia mtandao huu kuwa Jonas Mkude ataendelea kuwa chini ya uangalizi maalumu wa kitabibu huku akifanya mazoezi ambayo ni mepesi kwa muda huu .

“Ataendelea kuwa chini ya uangalizi maalumu wa kitabibu huku akifanya mazoezi mepesi ambayo hayatoweza kumfanya apate majeraha tena kwa mara ya pili” alisema daktari huyo wa Simba.

Sambaza....