Wananchi watashuka dimbani keshokutwa Jumatano ya Machi 8 mwaka huu kuvaana na Real Bamako kutoka Mali katika mchezo wa nne wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika kundi D.
Mpaka sasa Yanga wana alama nne ambazo zinaweka matumaini yao hai ya kufuzu robo fainali ya michuano hiyo kwani wapo nafasi ya pili nyuma ya kinara US Monastir mwenye alama saba.
Mchezo wa Yanga utapigwa siku ya Jumatano na itakua ni siku ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka ya tarehe nane mwezi Machi.
Kutokana na siku hiyo kuangukia siku ya mchezo wao, Yanga wametoa uwanda mkubwa kwa mashabiki, mashirikia na watu binafsi kununua tiketi nyingi ili kusaidia wanawake kujumuika kwa wingi katika mchezo huo.
Na tayari muitikio mkubwa umeonekana huku baadhi ya mashirika na watu binafsi wakinunua tiketi 100 mpaka 300 kwa wakati mmoja ilo zigawiwe kwa wanawake wataokwenda katika mchezo huo.
Baadhi ya wanachama wa Yanga walionunua tiketi 100 ni pamoja na Anthony Mavunde na Crispo Hezron. Pia mashirika na kampuni mbalimbali kama Kangaroo Insuarance Brookers, Jembe Energy Drink na Feedlance wamenunua tiketi 100 na 300 kuelekea mchezo huo.
Yanga watashuka dimbani wakiwa na nguvu ya mashabiki hap watakaojitokeza katika Dimba la Benjamin Mkapa na hivyo kuzidi kuongeza nafasi yao yakupata ushindi mbele ya wapinzani wao Real Bamako.