Ibrahim Ajibu Migomba ni kama ameweka rekodi ya wajina wake Zlatan Ibrahimovic ambae kwa sasa yupo Marekani katika Major League Soccer (MLS).
Uhamisho wa Zlatan Ibrahimovic kutoka Inter Milan kwenda FC Barcelona ni kama alipishana na kombe lá Ligi Ya Mabingwa Ulaya baada ya Inter Milan kubeba kombe hilo na Barcelona kutoka mikono mitupu.
Ni kama kilichomkuta pia Ibrahim Ajibu baada ya kuukosa ubingwa Simba na kuamua kwenda Yanga msimu huu, na Kumfanya apishane na kombe la Ligi Kuu Bara msimu huu baada ya Simba jana kutangazwa mabingwa wapya.
Ibrahim Ajibu alianza na klabu ya Simba katika kikosi cha Timu B mpaka kuwa mchezaji tegemeo katika klabu ya Simba hiyo, mpaka pale alipoamua kuhamia kwa mahasimu wao Yanga waliokua wametwaa ubingwa wa VPL misimu mitatu mfululizo.
Kutokana na matokeo ya Tanzânia Prisons dhidi ya Yanga jana kumeifanya Simba kuchukua ubingwa wakiwa kwenye “makocha”. Hivyo kumfanya Ibra Cadabra atoke kapa msimu huu kama wajina wake Zlatan Ibrahimovic.