Klabu ya soka ya Yanga leo kupitia mkutano mkuu wa klabu wamemtambulisha kocha wao mpya Miguel lAngel Gamondi kuwa mrithi wa Nasraddine Nabi aliyeachana na klabu hiyo.
Miguel 56, akiwa na uraia wa Argentina na Italy pia si mgeni Afrika kwani ameshavifundisha vilabu vingi barani Afrika, akikaa Afrika kwa takribani miaka 20.
Kocha huyo Muargentina amevifundisha vilabu kama Wydad Casablanca, Mamelodi Sundowns, Esperance de Tunis, USM Algier, CD Beloizdaid na Platinum Fc.
Mara ya mwisho Migeul alionekana na klabu ya Ittihad Tanger kabla ya kuachana nayo April mwaka jana na sasa amejiunga na Wananchi Yanga waliotoka kupata mataji mfululizo ndani ya miaka miwili wakiwa na Mtunisia Nabi.
Miguel sasa ni wazi anapaswa kuanzia alipoishia mtangulizi wake Nasraddine Nabi aliyedumu kwa miaka miwili na nusu na kuwapa Yanga mataji sita.
Kocha huyo ametumia muda wake mwingi akifundisha timu za Kiarabu huku akiwa ni muumini mkubwa wa mfumo wa 4:2:3:1 na mara chache amekua akitumia 4:3:3.