Sambaza....

Klabu ya Azam Fc imekamilisha usajili wa mshambuliaji Alassane Dialo kutoka klabu ya US Goore ya Senegal kwa mkataba wa miaka miwili.

Nyota huyo akiwa bado kinda anakwenda kuungana na washambuliaji wazoefu Prince Dube na Idris Mbombo ili kwenda kuunda safu mpya ya ushambuliaji ya Azam Fc. Tazama hapa jinsi Zaka za Kazi, Zakaria Thabit alivyoitanabaisha wasifu wa nyoa huyo Msenegali.

Watu wanachanganya jina la mchezaji mpya wa Azam FC, Alassane Diao(tamka Jao), na jina la mchezaji mwingine Alassane Diallo ((tamka Jalo).

Wachezaji wote wawili walikuwa klabu ya US Gorée ya Senegal. Alassane Dialo ndiyo nahodha, na Alassane Diao ni mshambuliaji chipukizi mwenye miaka 20 sasa.

Huyu wa pili ndiye aliyejiunga na Azam FC, yaani Alassane Diao, siyo yule wa kwanza yaani Alassane Dialo ambaye ni nahodha. Huyu aliyejiunga na Azam FC ni dogo aliyekulia kwenye akademi kubwa zaidi nchini humo ya Generetionfoot.

Huu ni msimu wake wa tatu kwenye Ligi Kuu, baada ya mmoja akiwa na timu yake ya akademi na miwili akiwa na US Gorée. Misimu yake miwili ya mwisho amecheza mechi 25 na kufunga mabao 13 na assist 7.

Alassane Diao

2021/22

Alicheza mechi 15
Alifunga mabao 8
Akatoa assist 3

2022/23

Amecheza mechi 10
Amefunga mabao 5
Ametoa assist 4.

Ligi ya Senegal bado inaendelea na sasa iko katika mzunguko wa 23, katika mizunguko 26 ya msimu mzima.

Alassane Diao alikosa mechi nyingi msimu huu kutokana na kuja Tanzania kufanya majaribio Azam FC kwa takribani mwezi mzima.

Baada ya kufuzu majaribio ndiyo akarudi kwao kuendelea na ligi, lakini kwa kuwa huku timu yake mpya inaanza maandalizi ya msimu ujao, akabidi aje baada ya klabu zote mbili kufikia makubaliano na kusaini mkataba wa miaka miwili.

Sambaza....