WAPWA: wakati tunasubiri muda uende game ya @simbasctanzania iwadie,tu by time kwa story hii
Nilipo post juu ya kiatu cha ‘bahati ‘katika career ya soka wengi walikuja DM na kudadisi vitu kadha wa kadhaa kuhusiana na dhana hiyo
Lakini ukweli utabaki kuwa hiyo ni imani ya kisaikolojia inayojengwa na ushuhuda ( Ashahadu) za kitakwimu
Je ni kweli baada ya kukivaa kiatu hicho unachoamini kina bahati ulifunga magoli mangapi katika mechi ngapi?
Na mara baada ya kuacha kukitumia hufungi magoli au unafunga ama inakuaje kuwaje? Lazima uthibitishe kwa ushahidi wa kitakwimu pia
Pichani ni kiatu cha bahati pia kama nilivyopata bahati ya kutembelea jumba la makumbusho ya soka tu Germany iliyopo mji wa Dortmund.
Katika makumbusho haya kulikuwa na vitu vingi vya kuvutia ,mimi hupenda kusema vitu ” laki sita milioni” kuonesha uwingi usio na kifani
Moja ya vitu hivyo ni pamoja na kiatu hicho unachokiona kwenye picha ,ni kiatu cha mguu wa kushoto kilichovaliwa na Mario Gotze kwenye mchezo wa finali ya kombe la Dunia mwaka 2014 Brazil
Fainali iliyohusisha Germany vs Argentina
na kumalizika kwa ushindi wa bao 1-0 kwa upande wa Germany
Huku goli hilo muhimu likifungwa na Mario Gotze dk 113 baada ya kuwa suluhu katika 90′ na kwenda muda wa nyongeza
Gotze chipukizi wa wakati huo akiwa miaka 22 tu aliingia mwishoni mwa mchezo dk 88 kumpokea mkongwe Milasovik Klose na kuwa shujaa wa mchezo kwa kile alichokifanya ,huku akififisha matumaini ya Lionel Messi kunandika historia yake ya kutwaa ubingwa huo muhimu kwenye Career za wacheza soka
Hicho ni kiatu cha mguu wa kushoto ,cha mguu wa kulia ambacho ndiyo alitumia kufungia kiliuzwa kwenye mnada kwa ajili ya kuchangia mifuko ya hisani kwa Euro ambazo ukizihamisha kwa fedha ya Kitanzania ni zaidi ya Billion 5
Kwa upande wa mchezaji mwenyewe Mario Gotze pamoja na kuanza vizuri kama hana mwisho mzuri baada ya kucheza Bayern Munich na Dortmund alitarajiwa kuja kuwa mchezaji mkubwa zaidi duniani lakini haijawa hivyo
Kwa sasa anacheza PSV ya Uholanzi akiwa kwenye kiwango cha kawaida kutoka kufikiriwa kuja kushinda Ballon d’or pamoja na yote kuna kitu cha kujifunza
Weekend Njema!