Rufaa ya aliyekuwa Makamu wa raisi wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Michael Richard Wambura, inataraji kusikilizwa kesho Jumamosi Machi 31, 2018 katika ofisi za Shirikisho hilo
Kwa mujibu wa Wakili Emmanuel Muga anayemtetea Wambura, alisema kuwa wameshapokea barua ya kuitwa inayomtaka Wambura aende na utetezi wa maandishi ama njia ya mdomo ili kukamilisha usikilizwaji wa rufaa hiyo
Kamati ya maadili ya Shirikisho hilo ilimfungia maisha Wambura, kutojihusisha na soka nchini baada ya kukutwa na makosa matatu ya kinyume cha maadili ya Shirikisho hilo, ambapo Wambura alikata rufaa kunako kamati ya rufaa ya maadili ya TFF
Rufaa hiyo, inataraji kuanza kusikilizwa majira ya saa 5:00 asubuhi kunako ofisi za Shirikisho hilo zilizopo Karume Ilala jijini Dar es salaam