Kiungo mjerumani na anayelipwa mshahara mrefu zaidi ndani ya washika mitutu wa London,Arsenal, Mesut Ozil yuko sokoni kwa sasa, na muda wowote huenda akatimkia kusiko julikana.
Ozil ambaye alipata nafasi ya kuanza katika michezo 11 pekee kati ya michezo 26 ya Arsenal, alifunga magoli 3 na kutoa pasi 1 ya mwisho EPL msimu huu chini ya kocha mpya, Emery Unai anaidaiwa kutokuwa katika mipango ya kocha na klabu ipo tayari kumuuza na hata kumtoa kwa mkopo katika dirisha la kiangazi.
Ikumbukwe kuwa, Ozil alisaini mkataba mrefu msimu uliopita wa na kumfanya asalie hadi mwaka 2021. Arsenal kwa sasa inahaha kuipata klabu itakayokubali kumnunua kuendana na thamani yake. Ozil hadi sasa ana miaka 30, na inaonekana kiwango chake si kizuri kiasi cha kumuweka sokoni.
Klabu yake imedai kuwa, endapo kama itakosekana klabu ya kumnunua, klabu ipo tayari kumtoa kwa mkopo, kwakuwa ni vigumu kubaki na mchezaji asiye katika mipango ya kocha.
Mesut Ozil tangu asaijiliwe kutoka Real Madrid, ameifungia Arsenal magoli 30, katika mechi 153 alizocheza . Katika michezo hiyo, ni mechi 88, arsenal iliibuka na ushindi, ikipoteza mechi 32. Magoli aliyofunga Ozil ni wastani wa goli 0.21, magoli ya vichwa 4, mguu wa kulia 4 na mguu wa kushoto magoli 22, mpira wa kutenga goli 1, miaka yote hiyo amepiga mashuti 190 na yaliyolenga goli yakiwa 86, ikiwa ni asilimia 45, ya usahihi wa mashuti yake.
Ozil kama kiungo mshambuliaji hadi sasa ameshatoa pasi za mwisho 51, pasi za kawaida 9,721, ikiwa ni wastani wa pasi 63.5 kwa kila mechi aliyocheza.
Kinidhamu Ozil yupo vizuri, hadi sasa hajawahi pata kadi nyekundu hata moja, njano anazo 11, amefanya madhambi mara 76 na ameotea mara 71.
Pia ni mzuri katika kutekeleza jukumu la ulinzi, hadi sasa tayari ameshafanya “tackles” 140, akifanikiwa kwa asilimia 71, amezuia mashuti na mashambulizi 52.
Rekodi zote hizo za Ozil bado hayupo katika
mipango ya kocha mpya, Unai Emery.