Baada ya kupokea kichapo cha mabao mawili kwa sifuri kutoka kwa JS Saoura katika mchezo wa Klabu Bingwa Africa msemaji wa klabu ya Simba leo mchana amezungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa mwisho dhidi ya AS Vita.
Ikumbukwe klabu ya Simba inahitaji ushindi pekee ili kuweza kufuzu hatua ya robo fainali kutokana na msimamo wa Kundi D jinsi ulivyo ambapo sasa Simba inaburuza mkia ikiwa na alama 6.
Haji Manara “As Vita ni klabu nzuri nimetazama mchezo wao dhidi ya Al-Ahly wamecheza vizuri haswa kipindi cha pili na walitufunga goli tano tunalijua hilo. Lakini hata Al-Ahly walitufunga goli tano na tukaja tukawabidua hapa.”
“Pale kwa mzee Mkapa pale kwenye Champions League kutoka labda uje na vifaru au mizinga. Lakini ili tushinde mechi hiyo tunahitaji watu elfu sitini (60,000) ili wahanikize. Lazima tuimbe, lazima tucheze na lazima tuwazomee Wacongo ili tushinde. Wale Saoura walikuja hapa wakakutaa uwanja umejaa wakashangaa na kuanza kupiga selfie na mashabiki mana hawajawahi kukuta uwanja umejaa vilee, wakala tatu hapaa.” Hajji Manara aliongeza.
VIINGILIO VYATAJWA.
Manara pia katika mchezo huo alitangaza viingilio vya mchezo huo. Katika mchezo huo viingilio vitakua:
Mzungunguko 3,000
V.I.P B 10,000
V.I.P A 20,000
Platinum 100,000.