Sambaza....

Kwanza unapaswa kumlaumu mlinzi wa Mbao Fc, Amos Charles . katika mazingira ambayo hakuwa katika presha yoyote anapoteza kujiamini- sijui kwanini wakati katika mtazamo wangu wa kimpira walitawala mechi ya jana katika uwanja wa Taifa.

Kwa mlinzi ambaye timu yake ilicheza mbali na goli lake huku wakipokea mashambulizi machache yaliyokosa ubunifu, Amri Said kama kocha amepata jibu la kuanza kutazama timu yake katika eneo la ulinzi. Alikuwa beki mahiri enzi za uchezaji wake, lakini anapaswa kmaliza tatizo la uoga kwa safu yake ya ulinzi wa kati ili aendelee kufanya vizuri.

Waliibana sana Yanga SC, eneo la kati ambalo Yanga waliwaweka Feisal Salum, Deus Kaseke na mfungaji wa goli lao la kwanza Fafael Daud; wakisaidiwa na Matheo Anthony na mfungaji wa goli la ‘video’ Ibrahim Ajib, Amri alishuhudia timu yake ikitawala mchezo kwa robo saa yote ya kwanza licha ya awali kuonekana Amri ameipeleka timu yake –kujilinda.

Baada ya kuona wamemudu mchezo, Amri akaamua kubadili aina ya uchezaji na mabadiliko yake ya kwanza dakika nne kabla ya mapumziko yalimaanisha anataka kukomboa goli la Dau ambalo lilifungwa dakika ya 16’ akiunganisha kwa kichwa mpira wa faulo uliopigwa na Ajib.

Golikipa Hamim Mussa alitokea vibaya mpira liopigwa kwa stahili ya ndizi, na bahati mbaya kwake kila alipokuwa akiifuata anajikuta yupo mbali na goli huku mpira ule ukienda kwa mlengwa. Ni goli zuri alifunga Daud lakini ili nalo lilitokana na uwezo mdogo wa golikipa huyo wa Mbao FC katika usomaji wa mipira iliyokufa.

MPE SASA SIFA ZAKE AJIB

Mara baada ya kuumia kwa Beno Kaklanya dakika kumi baada ya kuanza kipindi cha pili na kuingia golikipa Mcongo, Klasus Kindoki- Yanmga kama timu-kama klabu wote waliingia katika hofu. Ndani ya dakika tano hata Kindoki mwenyewe alishindwa kujiamini hilo likaongeza presha.

Wakati mechi ikiendelea huku matokeo yakiwa Yanga 1-0 Mbao na vijana hao wa Amri wakifanya mashambulizi kadhaa mazito, Vicent Andrew naye anaumia mechi ikikaribia robo saa ya mwisho. Presha inaongezeka zaidi kwa sababu kocha Noel Mwandila analazimika kufanya mabadiliko mawili ya lazima kwa safu yake ya ulinzi.

Katika hali ya kawaida ya kimchezo inachanganya sana hata kwa wachezaji hasa ukizingatia tayari Matteo alikuwa ametotolewa dakika ya 57’. Kama uliona namna meneja Nadir Haroub alivyoshangilia na kocha wake Mwandila baada ya bao kali ‘tik tak’ ya dakika ya 90+2’ basi elewa lilishusha ile presha waliyokuwa nao watu wa Yanga.

Ajib amejidhihirishia kuwa yupo katika mabadiliko makubwa kiuchezaji, alitumia makosa ya mlinzi wa Mbao kuondoa mpira bila uelekeo na alivyojigeuza na kushuti akiwa amelipa mgongo goli hilo ni kielelezo kuwa sasa yupo fiti kimazoezi, na sasa haya ndiyo majibu mazuri kwa zile ‘fimbo’ tulizomchapia wakati ule tukimuita mvivu wa mazoezi, lakini haitoshi.

Magoli mawili, pasi sita za magoli katika michezo sita, Ajib anahitaji kuendelea kujibiidisha katika mazoezi, narejea tena huyu ni namba kumi wa kipekee lakini ni mvivu na asiye jail kupoteza pasi mchezoni. Goli lake vs Mbao FC jana Jumapili liwe mwanzo tu wa kuendelea kufunga yake yake ya kuvutia . tunasema, ‘Bonge la Goli’

Sambaza....