Baada ya mkanganyiko wa mechi ya fainali ya pili ta Ligi ya Mabingwa Afrika 2018/2019 kati ya Esperance na Waydad Casablanca na kupelekea mechi kusimamishwa, rais wa Caf Ahmad Ahmad aliitisha kikao cha dharula cha kamati kamati kuu tarehe 4 mwezi huu kujadili zaidi.
Agenda kuu ya kikao hicho ni kutafuta majibu kuhusu kanuni zinazohusiana na mechi.
Ikimbukwe katika fainali hii, mechi ilishindwa kuendelea baada ya kutokea malalamiko ya goli ambao halikuweza kuthibitishwa na VAR (Teknolojia ya Video), Waydad Casablanca waligomea kuendelea na mechi hivyo CAF kutoa uamuzi wa Esperance kupewa ushindi huo.
Je fainali ya ligi ya Mabingwa mechi ya pili inaweza rudiwa?
Katika kanuni za Ligi ya Mabingwa zilizotoka 2018, sehemu ya XII. INTERRUPTED MATCHES ipo kimya kuhusu mazingira yalioyopelekea mechi hii kuahirishwa. Na huenda hii ndio sehemu itakayorekebishwa ili kuondoa utata huo.
Maamuzi haya yanaweza kutoa mwanga kwa nini kifanyike katika mazingira kama yaliyotokea katika mechi hii, kupunguza lawama na kuongeza imani kwa timu shiriki. Taarifa rasmi ya kikao hicho bado hazijatoka, pindi tu zikitoka tutawaletea.
Taarifa, tulizozipata usiku huu ni kwamba Esperance wanatakiwa kurudisha Kombe na Medali kwaajili ya marudio ya fainali ambayo itafanyika nchini Misri baada ya michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika. Zaidi tutawaletea…….