Sambaza....

Kuna usemi usemao ” Simba akikosa nyama hula majani”. Usemi huu unasadifu ile dhana ya maisha “kukosa na kupata” . Licha ya kuwa Simba ni hodari wa mawindo lakini kuna nyakati huwa ngumu kwake kwani hata yale mawindo marahisi (mepesi) pia hukosa na kuambulia patupu.

Dhana hii inaakisi maisha ya Simba Sport Club kwa miaka mitatu mfululizo ya kuvikosa vikombe vya Ligi Kuu NBC na Azam Confederation Cup. Kabla ya miaka hii mitatu ya hivi karibuni ya kukosa vikombe, Simba Sports walikuwa katika kipindi kizuri cha mawindo kwani walifanikiwa kuwa mabingwa wa ligi kuu mara nne mfululizo.Kama ilivyo asili ya mbuga Simba ndiye mfamle na hodari wa mawindo, na katika soka la Tanzania.

Simba Sports wanajinasibu kuwa hodari katika kutandaza kabumbu kwani mara zote wamekuwa wakifanya vizuri ndani na nje ya nchi. Kwa sasa Simba wanapitia kipindi cha mpito, wanapambana kutaka kurudi katika ubora wao kwani kwa misimu mitatu mfululizo ya hivi karibuni wameshindwa kufanya vizuri katika ligi kuu Tanzania bara.

Msimu huu wa ligi ya NBC 2024/25, Wamefanya usajili mkubwa wa wachezaji hususani wachezaji vijana umri kati ya miaka 21-27. Isitoshe wamefanya mabadiliko katika benchi la ufundi kwa kuleta benchi jipya la ufundi ambalo liko chini ya muafrika kusini FADLU DAVIS.

Katika kipindi kifupi kocha Fadlu ameibadilisha Klabu hii kwa kiasi kwani ameongeza hali ya ushindi na ushindani. Simba imeanza ligi vizuri kwani katika michezo kumi ya ligi kuu, ushindi 8, sare 1 dhidi ya Coastal Union na kupoteza 1 dhidi ya Watani zao Yanga huku wakijikusanyia jumla ya alama 25 wakiwa juu katika msimamo wa ligi kuu NBC kwa tofauti ya alama 1.

Kocha Fadlu Davis ni kocha anayejituma sana na kazi yake ndio maana kwa mda mfupi amefanikiwa kuibadilisha Simba na kuifanya icheze kwa nmna yake. Fadlu ni muumini wa DIRECT FOOTBALL. Yaani mpira wa kasi na moja kwa moja usio na pasi nyingi, lakini amekuwa akibadilika kutokana na mazingira ya kila mechi kutegemeana na mazingira ya mchezo.

PosTimuPGDPts
1151533
2122131
3121330
4141130

Kinachombeba ni uwezo wake mkubwa wa kimbinu na uwepo wa wachezaji wengi vijana wenye nguvu na vipaji vikubwa ambao wako tayari mara zote kubadilika ili kukidhi mahitaji na matakwa ya bechi la ufundi katika kila mchezo. Wakiwa na wastani wa asilimia 80% ya ushindi katika michezo 10 ya ligi mpaka sasa, wakifunga magoli 21 na kuruhusu magoli 3 pekee ikiwa na wastani wa goli mbili kwa kila mchezo.

Mabadiliko haya ya haraka na ya mda mfupi yamekuja kurudisha imani ya mashabiki kwa timu yao na kuamini kuwa msimu huu ni msimu wa ubingwa kurudi mikononi mwao baada ya miaka mitatu ya ukame.Licha ya kufanya vizuri na falsafa yake kujionyesha ndani ya muda mfupi lakini Simba iliyopo kichwani mwa Fadlu bado haijatimia, ni kama nusu ya kile kilichopo kichwani mwake(50%).

Kushambulia kwa nguvu

wachezaji wenye nguvu na kasi kubwa katika maeneo yote ya uwanja wenye uwezo wa kushambulia na kuzuia kwa kasi katika muda wote wa mchezo (Dakika 90).

Kujitoa na kupambana kwa asilimia 100% muda wote mchezoni.

Kwa kuzingatia haya na kwa kulinganisha na kikosi cha Simba cha sasa, aina ya wachezaji wake wengi ni wazuri sana katika kushambulia kuliko kuzuia, wapo wachezaji kadhaa wanakubalika na falsafa hii ya kushambulia kwa kasi na nguvu kama vile Kibu Denis, Ladack chasambi, Joshua mutale. Licha ya kufanikiwa na kuanza kujionyesha lakini Falsafa hii imeonyesha madhaifu machache katika mechi hizi chache za Ligi. Madhaifu haya hayajaonekana sana ila yanaonekana endapo Simba watakutana na;

Timu Iliyo vizuri kwa mashambulizi ya kushitukiza :

Wachezaji wengi wa Simba ni wazuri katika kushambulia kuliko kuzuia hivyo ikikutana na timu iliyojengeka vema kwa mashambulizi ya kushtukiza basi Simba itaadhibiwa. Kwamfano mchezo dhidi ya coastal union pale KMC complex uliomalizika kwa sare ya goli 2-2. Simba walikuwa wakiongoza kwa goli mbili kwa sifuri lakini wakajakufungwa goli mbili kwa mashambulizi ya kushtukiza tena kwa kupiga kutoka umbali mrefu na kulazimishwa sare.

Timu iliyo vizuri kuzuia mianya ya pasi:

Simba inapata wakati mgumu inapokutana na timu ambayo iko imara katika kuzuia mianya ya pasi wamekua wakishinda kwa tabu sana tena kwa ushindi finyu kwamfano mchezo dhidi ya Tanzania prison pale Sokoine na Ule dhidi ya mashujaa (wazee wa mapigo na mwendo) pale Lake Tanganyika Kigoma falsafa hii ilishindwa kufanya kazi ipasavyo bali yake walikuwa wakitegemea mipira iliyokufa na kufanikiwa kupata goli kwa mpira uliokufa katika dakika za jioni kwa goli la Dese Mukwala.

Fadlu Davids na Simba yake kama wanautaka UBINGWA wa ligi kuu NBC msimu huu watatakiwa kufanya ziada katika uwanja wa mazoezi kuwabadilisha waliopo ili waendane na falsafa yake japo itakuwa ngumu lakini inawezekana ama dirisha lijalo (dogo) warudi sokoni kutafuta wachezaji wa falsafa yake.

Sambaza....