Kutoka kwenye Sanduku langu la Maoni mpira ule haukuvuka mstari wa Goli na ndio maana leo hii kumetokea pande mbili zinazokinzana kuhusu kama lile lilikuwa goli halali ama la!
Kwa nilivyoona lile Tukio kwa Picha za Video tulizopewa toka Room ya VAR hazikutosha kusema lile ni Goli Halali!
Sheria namba 10 ya SHERIA YA GOLI KWENYE MCHEZO WA SOKA – IFAB wenye Sheria zao inasema “goli linafungwa na kukubalika endapo mpira wote (Usibaki hata kidogo) utakuwa umevuka mstari wa goli uliochini ya milingoti ya goli huku kukiwa hakuna uvunjifu wowote wa sheria za Soka kwa timu iliyofunga goli”
Ni Mstari wa goli “ULIO CHINI” Ukiangalia Video zote zinazotembezwa kwenye Magrupu ya Wasape na Mitandao ya Kijamii zinaonesha Mpira ulio Juu sasa kwatukio lile la ule Mpira Umedunda na Picha zilizokamatwa Mpira upo juu na sio kukaa kwenye Mstari na hapa sasa inakuwa Ngumu kuamua kuwa Lile ni Goli sababu kuna Angle ile Camera ilichukua ikaonesha kuwa Ule Mpira haujavuka Mstari ukiwa pale pale juu na kuna Angle ya pili inaonesha mpira umevuka!
Hakuna Mwamuzi Duniani anamua kwenye scenario ya vile! lakini pia Kuna kitu ambacho watu wote wanaofatilia Mpira wameamua Kuibebesha LAWAMA VAR kana kwamba VAR ile ni kazi yake ya Msingi!
Katika UTAMBUZI wa mpira kuvuka Mstari ama La hiyo sio Kazi Mama ya VAR ndio maana Wazungu walianza na GOAL LINE TECHNOLOGY! (GLT) hii ndio Teknolijia yenye Kazi Mahususi ya kutambua kama Mpira umevuka Mstari ama La!
Wazungu walianza na Suala la Mpira kuvuka Mstari GLT sababu lile ndio lilikuwa Jambo gumu zaidi kuamuliwa na Waamuzi wa ndani ya Uwanja kuliko Jambo lolote lile sababu ni kitu kinachotokea kwa umbali mkubwa sana kutoka kwa Mwamuzi na Wasaidizi wake wa pande zote mbili!
AFRICA sisi tumevuka Stepu na kwenda kwenye VAR kabla ya GLT sababu Sisi tuna makosa mengi sana ambayo katika kuyahalalisha tumeyapa jina “Makosa ya Kibinadamu” hasa linapokuja suala la Utambuzi wa Offside
Kwa Wazungu VAR inatumika kwenye maeneo haya Matatu
- Offside
- Kutoa ama Kufuta Adhabu Kubwa (Red Card) ikitokea Mwamuzi kafanya maamuzi kwa makosa; na
- Kuangalia kama kulikuwa na tukio lolote lile lisilo la kiungwana kabla ya goli kufungwa ama kama kuna namna mchezaji alifanya makosa yakiyopaswa kuadhibiwa na Refa hakuyaona hapa kuna matokeo mengi huwa yanatokea
a) Kufuta Goli kama lilifungwa baada ya makosa kutokea ambayo refa hakuyaona
b) Kuhalalisha Goli lililofungwa ikiwa Refa alilikataa at first place kwa makosa
c) Ku Award ama Kufuta Penati kama haku-Award ama Ali-Award at first sight kimakosa!
Kama hayo yote yapo sawa basi hutaweza kuona VAR ikiamua Mpira kuvuka ama kutovuka Mstari!
FACT NI KWAMBA
Mwamuzi wa Mchezo husika Hakuwapa Yanga Goli baada ya mpira wa Aziz Ki aliruhusu mchezo kuendelea sababu hakupata Taarifa ya kuwa lile ni Goli kutoka kwa msaidizi wake ambaye nampa benefit of doubt kwasabu asingeweza kuamua kutoka mahala aliposimama akiwa na last second defender wa Mamelodi ila ningeweza kumlaumu kwa kushindwa kuamua chochote kama angekuwa sambamba na Mstari wa Goli!
Hivyo sasa msaada pekee uliokuwa umebaki pale ambao huwezi kuutegemea kwa 100% kwa Facts nilizotoa huko Juu kukupa Maamuzi sahihi ni VAR – Team ya VAR ambayo ilikuwa chini ya Waamuzi watatu Waka Review Tukio Zima na kukubaliana na Maamuzi yaliyochukuliwa na ON FIELD REFEREE! Sasa kama Walikubaliana na Maamuzi ya Refa maana yake ni ku resume mchezo uendelee!
DHANA TOFAUTI
Kumeibuka Dhana TOFAUTI kwamba VAR haikutumika IPASAVYO nimejaribu kuwauliza watu wote waliokuja na Hoja hii wanipe maana halisi ya VAR kutokutumika IPASAVYO hadi muda huu sijapata Maana sahihi kabisa!
Kinachonisikitisha Wengi wao walioibua Hoja hiyo ni watu ambao huwa tunatazama nao Mpira mara zote na kuamini kuwa wana Upeo mkubwa sana wa utambuzi wa mambo madogo madogo lakini sababu Inagusa HISIA zao za MIOYO wanaweka Ufahamu wao pembeni!
Swali ni wakati gani Muamuzi anawiwa kwenda kupata Msaada wa VAR?
Majawabu ni kuna Matukio kama Matatu ambayo ni ya Msingizi zaidi huwa yanamfanya Mwamuzi wa Kati kwenda Kupata msaada wa VAR!
- Refa wakati anapotokea kuamua jambo lolote ndani ya Uwanja lakini Waamuzi wasaidizi waliopo kwenye VAR Room wakirudia na kuona ipo haja ya Refa kutazama upya Maamuzi yake kama alikuwa sahihi baada ya wale wasaidizi wa VAR room kutilia mashaka – Refa atawajibika kwenda kuangalia upya anaweza kukubaliana nao ama kutokukubaliana na wazo linalotokana na VAR kwenye mechi ya Mamelodi vs Yanga lilitokea Tukio lililomuhusu Joyce Lomalisa kucheza mpira na kuonekana Mguu wake ukimkwatua Sailor Khuliso Mudau VAR ilileta Opinion kuwa ile ilikuwa ni Dangerous Play so ilipaswa kuwa reviewed Refa akaenda kuangalia akasimama kwenye Maamuzi yake!
- Refa anapishindwa kufanya maamuzi ya Tukio lililotokea Uwanjani either kwa kutopata Clear view ama kuona haikupaswa kuchukua Hatua yoyote – VAR Room baada ya Ku Review Tukio Husika na kama wakajiridhisha kuwa Refa alifanya Makosa basi watamshauri kwenda kwenye VAR kuliona tukio husika kwa ukaribu na katika angle tofauti Ili maamuzi sahihi yachukuliwe!
- Lakini pia ikitokea Mwamuzi hakuamua na kukatokea Split opinion kwenye VAR Room kati ya wale waamuzi wasaidizi let say wawili wakasema mpira uendelee na mmoja akasema hapana hebu tupate kulitazama upya basi Refaree atapaswa kwenda kwenye Screen iliyopo uwanjani kuona kama anaweza kuamua vingenevyo ama kubaki na maamuzi yake ya Awali!
Kwenye Dhambi ya Udanganyifu Binadamu huwa anahukumiwa na Nafsi yake kwanza kabla ya kuamua kudanganya – Penati ya Nne jana usiku ya Asec vs Esperence Ilipopigwa mpira ukagonga Mwamba na kutua ndani ya mstari wa Goli wachezaji husika muda ule wote walipigwa na Butwaa kwanza sababu Dhambi ya Uongo huwa ngumu sana kuiigiza halafu baada ya sekunde kadhaa Wakati hadi Refa hakujua afanye nini pia Msaidizi wake ambae muda ule alikuwa sambamba na Mstari wa Goli nae hakujua afanye nini sababu yale mambo yanatokea kwenye kasi kubwa sana – Wachezaji wa Esperence wakamkimbilia kipa wao ambae aliwajoin kushangilia lakini VAR ilipoleta picha tukakubaliana Moja kwa moja kwamba Mpira ule ulivuka Mstari na CASE IKAWA CLOSED pale kwasababu hakukuwa na Chembe ya Shaka kuwa ule Mpira wote kuwa ulivuka mstari!
Anyway IT IS MY HUMBLE OPINION and from what i believe ni kwamba kama Ule Mpira ungeamuliwa kuwa ni Goli basi DUNIA ya Mamelodi na Waliokuwa wanawasapoti ingekuja na VIDEO na PICHA mnato ambazo zingekuwa zinaonesha namna walivyopigwa na DHULMA kauli ya Kocha Gamondi na Rais wa Utopwax!
Done and Dusted
©️The Writer😎