Kocha wa timu ya Asante Kotoko ya Ghana Paa Samuel Kwesi Fabin ameachia ngazi baada ya kudumu na mabingwa hao wa kihistoria wa Ghana kwa miezi saba.
Katika Barua aliyoandika asubuhi ya Leo akitaja sababu kubwa ya kuchukua uamuzi huo ni mambo binafsi na kusema kuwa ni wakati Mzuri kuchukua uamuzi huo kwani kwa sasa bado ligi imesimama na uongozi unaweza kutafuta mbadala wake.
“Ningependa kumshukuru Mwenyekiti mtendaji wa klabu kwa kunipa nafasi hii, uongozi wa timu, wachezaji na mashabiki kwa Upendo wao katika kipindi hiki tulichokuwa pamoja,” sehemu ya Barua hiyo imesema.
“Pia kwa wale wote ambao hatukupatana ama kutofautiana kwa maamuzi mbalimbali Ningependa kuwataka radhi kwani ni sehemu ya kazi,” amesema.
Fabin alichaguliwa kuwa kocha wa Asante Kotoko mwezi Februari mwakani huu kuchukua nafasi ya Muingereza Steve Polack ambaye aliachia ngazi baada ya timu kutolewa kwenye michuano ya kombe la shirikisho Afrika.