Klabu ya Everton imethibitisha kuwa itacheza na Mabingwa wa Kenya, Gor Mahia katika mchezo wa kirafiki Novemba 6 mwaka huu katika uwanja wa Goodson Park mjini Liverpool, England.
Everton wamethibitisha tarehe hiyo kwenye Mtandao wao wa Twitter.
Gor Mahia walipata nafasi ya kucheza na Everton baada ya kuwafunga Simba ya Tanzania kwa mabao 2-0 katika mchezo wa fainali ya SportPesa Super Cup uliofanyika mwezi Juni mwaka huu katika uwanja wa Afraha nchini Kenya.
Mwaka jana Eveton walikuja Tanzania mwezi Julai kucheza na Gor Mahia ambapo walifanikiwa kushinda kwa mabao 2-1 katika mchezo ambao ulifanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.