DO or DIE ndiyo kauli mbiu ambayo Simba wa wanaitumia kwenye mechi ya leo dhidi ya As Vita katika uwanja wa Taifa jijini Dar-es-Salaam. Mechi ambayo ina umuhimu mkubwa sana kwa Simba na Tanzania kwa ujumla. Ndiyo wawakilishi wetu kwenye hizi mechi za kimataifa.
Ndiyo watu ambao tunawatazama kwa kiasi kikubwa kama watu ambao watatupa furaha na sifa kubwa kwenye taifa letu. Sifa ambayo wameanza kuitengeneza tangu kwenye mechi za awali za ligi ya mabingwa barani Afrika mpaka hatua hii ya makundi.
Hatua ambayo wanaonekana wana nafasi kubwa sana ya kufuzu kwenda katika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya. Wanahitaji alama tatu tu. Uzuri ni kwamba hizo alama wanazihitaji katika uwanja wa nyumbani. Uwanja ambao kwao wamekuwa na matokeo bora kwenye michuano hii ya ligi ya mabingwa barani Afrika.
Wana asilimia mia (100%) ya matokeo katika uwanja wa nyumbani kwenye ligi ya mabingwa barani Afrika. Hawajafungwa wala kutoa sare kwenye uwanja wa nyumbani.
Hii ndiyo silaha ambayo wako nayo. Na hii ndiyo nguvu ambayo wako nayo, nguvu ambayo inawapa matumaini makubwa sana kwao wao kushinda mechi hii kwa sababu tu hawajafungwa msimu huu kwenye mechi za ligi ya mabingwa katika uwanja wa nyumbani.
Inaweza kuwasaidia ?, bila shaka inaweza kuwasaidia sana tena kwa asilimia kubwa kama wakiichukua katika mtazamo chanya.
Mtazamo ambao utawapa nafasi ya wao kutokujiamini sana kwa sababu tu ya uwanja wao wa nyumbani kujua kuutumia zaidi.
Lakini kama wakichukua katika mtazamo hasi , mtazamo ambao utawapa nafasi ya wao kujiamini sana. Wakijiamini sana kuna kitu kimoja ambacho kitatokea.
Kujiamini sana humfanya mtu anayejiamini afanye makosa binafsi. Makosa ambayo yanaweza kusababisha kuadhibiwa.
Tuachane na hayo turudi sasa kwenye kauli mbiu ya DO or DIE, kauli ambayo inatafasri moja ambayo mimi nimeielewa kwa upande wangu “KUFA au KUPONA”.
Hii ni tafasri ya kwanza, tafasri ya pili ambayo ni tafasri si si si unaweza kusema, kufanya au kufa. Hizi ndizo tafasri mbili ambazo unaweza kuzitumia na ukaendana sawa na mtazamo mkuu wa Simba.
Kauli hii mbiu kiukweli kwangu mimi naona ina udhaifu. Na udhaifu ambao unaweza kusababisha Simba kupata matokeo ambayo hayana nguvu ukilinganisha na kipindi cha nyuma.
Naamini sana kupitia kauli mbiu, naamini kabisa kuwa huwa zinatia moyo sana wachezaji kupigana. Ndiyo maana watu wengi huwa wanasisitiza kuhusu chakula cha akili.
Chakula cha akili ndicho humfanya mtu apigane, ndiyo humfanya mtu awe na morali kubwa ya kufanya kazi kutokana na kauli mbiu Fulani.
Yani kwa kifupi , kauli mbiu humfanya mtu aonekane ana deni kubwa sana ambalo hudaiwa na kauli mbiu husika.
Hivo lazima asimame kuitetea na kuipigania kauli mbiu husika kwa sababu tu ya kitu ambacho kinaonekana ni deni kwa kauli mbiu husika.
Simba walikuwa wanatumia kauli mbiu ya YES WE CAN. Kauli mbiu ambayo ilikuwa na nguvu sana. Kauli mbiu ambayo niliwahi kuwashauri Simba waitumie iwe wimbo wa Simba.
Kauli mbiu ambayo ilikuwa inatia nguvu sana kwa wachezaji wa Simba. Yani haikujalisha ugumu ambao upo kwenye macho yao lakini walikuwa na uwezo wa kufanya jambo imara.
Ugumu wowote haukuwepo kwao kwa ajili ya kuwazuia kufanya kitu ambacho ni imara, yani ugumu ulikuwepo pale kuhakikisha wanafanikiwa kupitia ugumu huo.
Ndiyo maana walifanikiwa kwenye mechi ngumu, alikufa Al Ahly hapa hapa Taifa kupitia kauli mbiu ile ile ya YES WE CAN.
Turudi kwenye DO or DIE. Kufa au kupona, kufanya au kufa. Yani hapa wamejichangulia matokeo mawili , yani wamejichagulia njia mbili za kupita.
Njia ya kwanza KUPONA/KUFANYA, njia ya pili KUFA. Njia ambazo wanatakiwa kuzikanyaga kwa wakati mmoja.
Yani mguu wa kulia ukanyage kwenye njia ambayo ni ya KUPONA/KUFANYA , afu mguu wa kushoto ukanyage kwenye njia ambayo ni KUFA.
Kikawaida huwezi kutembea kwa wakati mmoja kwa kukanyaga njia mbili. Yani mguu mmoja ukanyage njia Fulani, na mguu mwingine ukanyage njia nyingine.
Unajua kipi ambacho kinaweza kutokea ?. Hapo utaloose focus tu. Hutojua na target ya sehemu ambayo unaitaka. Utajikuta unakimbia kwa kasi bila uelekeo.
Kauli mbiu ambayo ingekuwa na uwezo wa kutia moyo ni ile ya YES WE CAN . Hii ndiyo kauli mbiu ambayo ilikuwa na nguvu kubwa kuanzia kwa mashabiki mpaka kwenye benchi la ufundi la Simba.
Hii ndiyo kauli mbiu ambayo ilikuwa inatoa nafasi kwa timu kutembea kwenye njia moja kwa kutumia miguu yote miwili.
Hii ndiyo kauli mbiu ambayo ilikuwa inatosha kutia morali kwenye mechi hii. Mechi ambayo ni muhimu kuzidi mechi yoyote waliyocheza msimu huu.
Hii ndiyo kauli mbiu ambayo itawakumbusha wachezaji kipi cha kufanya. Yani kimoja tu WANAWEZA KUFANYA MAAJABU. Kauli mbiu ya DO or DIE inawapa nafasi ya kuwa na machaguzi mawili, KUFA au KUPONA, Kitu ambacho siyo sahihi kwa sababu katika mechi hii Simba wanatakiwa Kufanya/Kupona na siyo kufa.