Hafsa habari wa klabu ya Yanga sc, Dismas Ten amesema kuwa sio jambo jema sana kujisifia kutoa sare ugenini kwa maana halikuwa lengo la kila mmoja
Akiongea kutoka makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Twiga na Jangwani, Ten alisema kuwa lengo ilikuwa ni kuona timu zinafudhu kwenda kunako hatua nyingine ya michuano wanayoshiriki
“Timu zetu zimetolewa nasema hivyo kama Mtanzania, kwa sababu tulikuwa na timu mbili ambazo zilikuwa zinawakilisha nchi salia kunako michuano mashindano mengine, lakini lengo lilikuwa ni kuona timu inafuzu kunako michuano ilikuyokuwa inashiriki mwanzo”
“Ifike wakati kwa sisi Watanzania kujiuliza tunataka nini kwenye vilabu vyetu na tunataka nini kwenye mpira wetu, kwa sababu tunahitaji kupata mafanikio, tunahitaji kushirikiana kunako njia moja ama nyingine kuhakikisha timu zetu zinafanikiwa”
Katika hatua nyingine Ten aliwataka wadau kutoa elimu kwa mashabiki kuvipenda vilabu vyao kutoka moyoni na sio bra bra
“Sisi wadau wa mpira, kwa maana ya waandishi umefika wakati sasa wa kuwandisha au kuwaambia ukweli mashabiki wetu, kupenda timu sio jambo rahisi kama ambavyo tunafikiri” alisema Hafsa habari huyo asiye na maneno mengi