Klabu ya Manchester city wanataraji kutoa ofa mpya kwa mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez 29, na wanaamini kuwa Arsenal wataruhusu raia huyo wa Chile kuondoka mwezi huu
Sanchez yuko tayari kurejea kima cha pauni milioni 25 kuhakikisha kuwa anajiunga na Manchester city
Arsenal watamruhusu Sanchez kuondoka endapo watapokea hadi pauni milioni 30, na wanataka mpango huo kukamilika mapema ili kuwawezesha kumtafuta mchezaji ambaye atachukua nafasi yake
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Sanchez huenda akajiunga na Manchester city kwa muda wa wiki moja inayokuja
Tayari Arsenal wamemuoridhesha mshambuliaji wa Monaco Thomas Lemar 22, kuwa namba moja kuchukuwa nafasi ya Sanchez, baada ya kushindwa kumsaini mfaransa mwenye uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani msimu uliopita