Timu ya taifa ya vijana ya Zanzibar iliyochini ya umri wa miaka 17, Karume boys, imeondolewa katika michuano ya vijana ya CECAFA yanaoyoendela nchini Burundi
Timu hiyo imeondolewa kufuatia kupeleka vijana 12, waliozidi umri huo suala ambalo ni kinyume na kanuni za mashindano hayo
Pamoja na kuondolewa, timu hiyo imetakiwa kulipa faini ya kiasi cha dola za Kimarekani 15,000 pia kurudisha gharama za tiketi huku ikifungiwa kutoshiriki mashindano hayo kwa kipindi cha mwaka mmoja
Karume boys, ilifanyiwa mabadiliko hivi karibuni ikiwa kambini ikijiandaa na mashindano baada ya kugundulika kuwa baadhi ya wachezaji kuzidi umri, lakini tatizo hilo limegundulika tena wakiwa nchini Burundi
Mbali na Zanzibar, Ethiopia nayo imekubwa na rungu kama hilo baada ya wachezaji wake kugundulika kuwa na umri wa zaidi ya miaka 17