Shirikisho la Kandanda Barani Afrika (CAF) limetangaza June 15 hadi Julai 13 kuwa Ndio tarehe rasmi ya kufanyika kwa mashindano ya Mataifa Afrika (AFCON).
Hata hivyo katika mkutano wake uliofanyika Sharm el-Sheikh nchini Misri jana, CAF imeshindwa kuthibitisha kama mashindano hayo yatafanyika nchini Cameroon Kama ilivyopangwa hapo awali.
CAF imesitisha kuitangaza Cameroon hadi mwishoni mwa mwezi November katika mashindano ambayo kwa Mara ya kwanza yatashirikisha jumla ya timu 24 badala ya 16.
“Maamuzi ya mwisho yatafanyika mwezi Novemba, wachunguzi wa CAF na FIFA watatumwa kwenda Cameroon mwezi Oktoba kuangalia hali ya usalama na miundombinu,” sehemu ya taarifa ya CAF imesema.
Pengine Morocco inaweza kuchukua nafasi ya kuandaa fainali hizo kama hadi November CAF itashindwa kuithibitisha Cameroon Kama mwandaaji wa mashindano hayo.