Pazia la ligi kuu Tanzania bara linakwenda kufunguliwa kwa mchezo wa Ngao ya jamii Wazungu wanaita’ community shield’ ukiwa ni kiashiria cha uzinduzi wa ligi.
Katika mchezo huo utawakutanisha Yanga na Simba uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa.
Yanga mwenyeji wa mchezo kwa kuwa anamiliki ubingwa wa mashindano Mama ya nchi yaani ligi kuu ( top tier league).
Simba anakuja kwenye mechi hii kikanuni zaidi baada ya kuwa makamu bingwa wa ligi kuu ya NBC kwa kuwa Yanga alikuwa bingwa pande zote mbili NBC na ASFC.
Nisema awike asiwike kutakucha game itapigwa ,mashabiki watapata wanachokihitaji kwa kuwa game hii haina sare lazima timu moja ife nyingine iibuke na ubingwa.
Tukiziangalia hizi timu mbili zinazokwenda kukutana jumamosi hii bila kuangalia rekodi za siku za nyuma.
Zote zipo vizuri kwa kuangalia vikosi vyao vya sana pamoja na maingizo mapya ambayo yameonekana ‘kuwaka’ kwa haraka kwenye mechi zao za wiki hii kwenye matamasha yao.
Kwa upande wa Simba Nelson Okwa na Augustine Okrah wameonekana kuleta chachu mpya ndani ya timu huku Mzungu Dejan Georgejavic akizua mjadala juu ya uwezo wake.
Kwa upande wa Yanga wao ingizo ambalo limepokelewa kwa furaha yawezekana asiwe Aziz Ki tena zamu ikawa kwa Gael Bigirimana aliyewavutia wengi akiwemo na Joyce Lomalisa.
Kwenye muunganiko wa timu kwa wachezaji wenyeji na wageni ,Simba kama wameenda haraka kwenye hili ukirejea michezo yao miwili ya mwishoni hapa.
Lakini kujipanga vyema ndiyo itakuwa jambo zuri zaidi na kufanyia kazi mapungufu ya upande wa pili unaoenda kukabiliana nao.