Baada ya kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” kutangaza kikosi cha wachezaji 31 kitakachoingia kambini kujiandaa na michezo miwili yakufuzu Afcon dhidi ya Uganda kuliibuka malalamiko kutokana na uteuzi wa kikosi hicho.
Miongoni mwa maeneo yaliyozua malalamiko ni katika walinzi wa pembeni ambapo Mohamed Hussein na Shomary Kapombe kutoka Simba hawajajumuishwa katika kikosi hicho.
Kw takwimu zilozotolewa na Bodi ya Ligi [TPLB] kwa msimu huu mpaka sasa Mohamed Hussein Zimbwe na Shomary Salum Kapombe ndio vinara katika kupiga pasi za mwisho miongoni mwa walinzi wote wanaocheza Ligi Kuu ya NBC.
Katika orodha hiyo Zimbwe na Kapombe ambao hawajajumuishwa katika kikosi cha Stars ndio vinara wakiwa na pasi tano za mabao kila mmoja mpaka sasa Ligi ikiwa imefikisha michezo 25.
Wanaofuatia ni Joyce Lomalisa wa Yanga mwenye pasi nne za mabao na Amos Charlea wa Geita Gold mwenye pasi tatu za mabao. Beki pekee aliyejumuishwa katika kikosi cha Stars anaeonekana katika orodha hiyo ni David Luhende kutoka Kagera mwenye pasi mbili tu za mabao.
Walinzi wengine wa pembeni walioitwa katika kikosi cha Stars Kibwana Shomary [Yanga], Datius Peter [Kagera Sugar] na Yahya Mbegu wa Ihefu wote hawapo katika orodha hiyo.