Kuna tetesi nyingi sana ambazo zilikuwa zimezagaa kwenye dirisha dogo la usajili kuhusu Beno Kakolanya.
Habari nyingi zilikuwa zimezagaa kuwa amevunja mkataba na klabu yake ya Yanga baada ya klabu hiyo kushindwa kumlipa mshahara wake na fedha yake ya usajili.
Leo hii mtandao wa Kandanda.co.tz umemtafuta Beno Kakolanya na amedhibitisha kuwa bado ni mchezaji wa klabu ya Yanga na hajavunja mkataba kama tetesi nyingi zinavyoenea kwa sasa.