Sambaza....

Kocha wa timu ya Taifa ya Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’ Stuart Baxter amemtangaza mwanae Lee Baxter kuwa kocha wa makipa wa kikosi hicho wakati ambapo wakijiandaa na mchezo wa kufuzu kwenye fainali za Mataifa Afrika dhidi ya Libya Jumamosi hii mjini Durban.

Lee Baxter ambaye ni kocha wa magolikipa wa timu ya Kaizer Chiefs amejuishwa kikosi na baba yake baada ya aliyekuwa kocha wa makipa Andre Arendse kutangaza kujiweka pembeni kutokana na Matatizo ya Kifamilia.

Shirikisho la soka la Afrika Kusini ‘SAFA’ limethibitisha taarifa hizo katika ukurasa wake wa Twitter kuhusiana na mabadiliko hayo madogo ya benchi la ufundi kuelekea katika mchezo huo muhimu wa kundi E.

Ikumbukwe kuwa Afrika Kusini katika mchezo wa kwanza wa kundi hilo waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Nigeria, huku Libya wakiwafunga Seychelles kwa mabao 5-1.

Sambaza....