Michuano ya Sportpesa imeanza kutimua vumbi leo mchana ambapo timu ya Mamlaka ya Bandari ya Kenya imefungua dimba dhidi ya Matajiri wa alizeti Singida united.
Katika mchezo huo uliopigwa saa nane mchana katika dimba la Taifa Bandari fc ya Kenya imefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali baada ya kuifunga Singida united bao moja kwa sifuri.
Bao pekee la Bandari fc katika mchezo huo limefungwa na William Wadri katika dakika ya 67 kwa njia ya mkwaju wa penati. Bandari walilapata mkwaju huo wa penati baada ya mlinzi wa Singida United Boniface Maganga kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.
Kwa matokeo hayo yanaifanya timu ya Bandari f c kufika hatua ya nusu fainali na hivyo kusubiri mshindi kati ya Yanga au Kariobangi Sharks.