Sambaza....

Mlinzi wa Mtibwa Sugar Abdi Banda ametoa maoni yake baada ya draw ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika  kuwakutanisha Simba na Orlando Pirates. Michezo hiyo miwili itapigwa April 17 na 24 ambapo Simba itaanzia nyumbani na kumalizia ugenini.

“Orlando Pirates wakija Dar es Salaam lazima watarajie mabaya na wajue vita itakuwa zaidi ya soka kwa sababu Simba inaungwa mkono na wanasiasa,” Banda alisema akinukuliwa na KickOff.

“Simba itamuweka mwamuzi mfukoni kwa sababu Simba itampa mwamuzi fedha. Simba huwa wanatumia mbinu chafu inapocheza nyumbani, lakini ni wazi hawana aina ya ubora unaolingana na Pirates hivyo watapanga bajeti ya kushinda nyumbani kwa tofauti kubwa.”  Aliongeza Banda ambae amcheze Ligi ya Afrika Kusini akivitumikia vilabu vya Baroka Fc na Highlands State.

Abdi Banda mchezaji wa zamani wa Simba sc na Coastal Union anaamini Orlando Pirates itafuzu na kuitoa Simba katika michuano hiyo.

Sadio Kanoute akichukua mpira mbele ya wachezaji wa Asec Mimosa

“Ninachojua ni kwamba Pirates itafuzu kwa nusu fainali baada ya mikondo miwili. Ingekuwa hatari kama Pirates wangecheza Johannesburg kwanza,” Banda aliendelea “Pirates lazima wamtumie Senzo [Mazingiza] kwa safari ya Tanzania kwa sababu anaifahamu vyema Tanzania na aliwahi kuwa Simba hapo awali na sasa yuko Yanga. Yanga watakuwa na furaha kuwasaidia Pirates kwa lolote wanalohitaji kwa sababu ni maadui na Simba.”

Klabu ya Simba imefakiwa kufika hatua yo robo fainali baada ya kumaliza nafasi ya pili katika kundi D nyuma ya RS Berkane na mbele ya Asec Mimosa na USGN.

Sambaza....