Stephane Aziz Ki. Ndio ni Young Africans ambayo inahitaji ubora na ufanisi wa miguu ya mtu huyu kuanzia katikati kwenda mbele ili kuzalisha kitu bora ndani ya uwanja.
Kuanzia kutengeneza nafasi mpaka ufungaji kwenye eneo la mbele! Yule Aziz KI wa msimu juzi pale Burkina Faso anahitaji kurudi tena kwenye macho ya watu.
Yule Azizi KI wa Asec Mimosas dhidi ya Simba SC kwenye michuano ya CAF watu wanahitaji kumuona tena! Ndio miguu yake inahitaji kutupa kitu bora zaidi ya msimu uliopita.
Matarajio ya watu kwa Aziz KI yalikuwa makubwa sana kutokana na kiwango alichoonesha kule alipotoka, dau la usajili lililotumika na uhitaji wa klabu kubwa dhidi yake wakati wa dirisha lile la usajili.
Timu inahitaji magoli na nafasi nyingi kutoka kwenye miguu ya Aziz KI! Feisal na Bangala wameondoka klabuni lakini Mudathir, Aucho, Zouzoua na Sure Boy wapo kwenye eneo hilo! Kwangu, naona Aziz KI akiwa kwenye ubora basi kuna kitu kikubwa kinaenda kuongezeka pale.
Rahisi. Msimu huu mwanga umeonekana kwenye mechi ya kwanza kwa Max Nzengeli hasa katika utengenezaji wa nafasi hivyo mimi naona Aziz KI kama miguu yake itakuwa na kitu bora sana basi Young Africans itazalisha magoli mengi sana.
Aziz KI msimu uliopita miguu yake iliamua mechi chache ndani ya uwanja, kwa msimu huu timu inahitaji kile akifanye kwenye mechi nyingi za msimu huu kuanzia mashindano ya ndani hadi nje.
Huu ndio msimu Stephane Aziz Ki kuonyesha kitu bora ambacho alikuonesha mpaka viongozi wa Young Africans SC wakawekeza pesa nyingi sana ili kukamilisha usajili wake.
Narudia tena! Endapo miguu yake itatoa kitu bora kama kama ilivyokuwa matarajio ya wengi basi naiona Young Africans bora kupitia miguu yake!