Sambaza....

Bruno Gomes Barossa! Msimu uliopita alikuwa kwenye kiwango bora sana kwenye mashindano yote aliyocheza akiwa na Singida Fountain Gate.

Ilikuwa ni ngumu sana kuzungumza ubora wa Singida FG pasipo kutaja Jina la Bruno Gomes! Kuanzia kutengeneza nafasi mpaka ufungaji alikuwa kwenye ubora mkubwa sana.

 

Msimu huu amechelewa kujiunga na wenzake ndani ya timu hali iliyopelekea kukosa baadhi ya michezo ya mwanzo lakini bado naona nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza.

Timu inaonekana kucheza vizuri ila bado inahitaji ubora wa Bruno Gomes ndani ya uwanja! Kama utaangalia vizuri kuna kitu kinapungua kuanzia eneo la kiungo kwenda juu. Kivipi?

Timu inapofanya “Transition” inatumia sana maeneo ya pembeni ambapo wanacheza Ambundo na Malouf Tchakei au Duke Abuya wanatanua uwanja ili kufungua njia zaidi huku Kagoma na Morris Chukwu pia ubongo wao ukiwa kwenye kupiga “Square Passes

Eneo la kiungo timu inamhitaji sana Bruno Gomes ili kupiga pasi nyingi mbele ya walinzi wa kati wa timu pinzani ( Central Backs )! Singida FG inahitaji kuwa bora kwenye “Transition” ili kutengeneza hatari nyingi mbele ya 18 ya mpinzani kuliko kutumia krosi zaidi.

Bruno Gomes.

Bruno Gomes kama anakuwa na dakika nzuri siku ni mchezaji ambaye atakupa kila kitu kuanzia kukaba, kutengeneza nafasi mpaka kufunga huku faida nyingine aliyonayo ni uwezo wa kupiga mipira ya kutenga (Set Pieces).

Hans Van de Pruijm kikosi chake kimefanya vizuri kwa baadhi ya mechi hizi za mwanzo lakini bado kuna namna naona wanahitaji ubongo wa Bruno Gomes ndani ya uwanja ili kuongeza ufanisi na idadi ya magoli kwa Singida Fountain Gate.

 

Sambaza....