- Safari ya Yanga, Mikononi mwa Dube
- Simba na Yanga nani anaongoza kuweka mpira kwapani.
- Yanga Waweweseka! Gamondi Nje!
- Fadlu Tunaamini anawapa Ubingwa Wekundu
- Manuel Neuer ana umri sawa na uchambuzi wa soka kwa kompyuta
Leo Biashara United inawakaribisha Simba ya Dar es Salaam katika uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara.
Biashara United inayonolewa na Amri Saidi ambaye tangu aichukue timu hii hajawahi kupoteza mchezo wowote katika uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara.
Akizungumza kuelekea mchezo huu mwenyekiti wa Biashara United, amedai kuwa maandalizi ya mechi hii yameshakamilika kwa asilimia kubwa.
“Maandalizi yameshakamilika kwa asilimia kubwa. Tunajivunia mashabiki wetu ambao huwa wanatupa nguvu kila tukicheza katika uwanja wa nyumbani. Mashabiki kutoka Tarime, Musoma na Bunda hutuunga mkono sana”.
“Na ukizitoa Simba na Yanga, timu pekee inayofuata kwa kuwa na amsha amsha ni Biashara United ya Mara. Kitu ambacho tunajivunia sana kwa sasa”.
“Sisi ni bora baada ya Simba na Yanga kwa hiyo mashabiki waje kushuhudia mechi nzuri”. Alidai mwenyekiti huyo wa Biashara United ya Mara.