Sambaza....

Dirisha la usajili rasmi limefunguliwa rasmi leo July moja na klabu ya Azam Fc kupitia msemaji wake Hasim Ibwe amesema watasajili wachezaji wanne pekee katika usajili wa dirisha huu huku mchezaji wa ndani akiwa Feisal pekee.

Hashim Ibwe akiongelea usajili alipokua akiongea na tovuti ya Kandanda.co.tz. alisema “Kwa wachezaji wa ndani hatutasajili mwingine ni Feisal Salum pekee mliyemuona,” alisema na kuongeza.

“Katika usajili wa dirisha hili tutasajili wachezaji wanne pekee, wawili tayari mmeshawaona huyu Sylla na wengine wawili wa Kimataifa tutawaongeza.”

Djibril Sillah usajili mpya wa Azam Fc

Ibwe alisema watasajili wachezaji katika eneo la ushambuliaji na eneo la mlinzi wa kushoto atakaechukua nafasi ya Bruce Kangwa huku pia akigusia jezi namba 10 ya Azam Fc msimu ujao.

“Tutaongeza mshambuliaji atakaekwenda kusaidiana na kina Prince Dube na Idris Mbombo pale mbele, ni mshambuliaji hatari makipa na mabeki wajiandae katika Ligi.”

“Upande wa mlinzi wa kushoto tunashusha chuma kwelikweli, subirini mtaona wenyewe ni “fullback haswa aisee. Tunamleta mlinzi kutoka nchi ya mpira haswa mtakuja kukumbuka maneno yangu.”

Ibwe pia aliiambia Kandanda.co.tz jezi namba 10 ya Azam Fc msimu ujao itavaliwa na chuma cha kuotea mbali waachane na wakata umeme sijui jezi namba sita kama inavyosemwa na watu wa Kariakoo.

Sambaza....