Sambaza....

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Kenya ya wanawake ‘Harambee Starlets’ David Ouma amekitaja kikosi cha awali cha wachezaji 32 ambao wataingia Kambini Jumatatu ya Oktoba 29 kujiandaa michuano ya Mataifa Afrika kwa Wanawake itakayofanyika mwezi ujao nchini Ghana

Kikosi hicho kitaingia kambini Jijini Nairobi na kitakuwa na wachezaji wawili walioongezwa wanaocheza soka la kulipwa Marjolene Nekesa anayecheza Marekani na Esse Akida anayecheza katika klabu ya Ramat Hasharon ya Israel.

Aidha katika majina hayo 32 wachezaji walioshiriki kwenye michuano ya CECAFA iliyofanyika mwezi Julai wameitwa wote ili kukipa uhai kikosi hicho kabla ya michuano hiyo ya wanawake maarufu kama AWCON.

Kikosi Kamili.

Makipa: Pauline Atieno (Makolanders), Maureen Shimuli (Wadadia), Annette Kundu (Eldoret Falcons), Monica Karambu (Thika Queens), Diana Tembesi (Wiyeta Girls)

Walinzi: Lilian Adera (Vihiga Queens), Wendy Achieng (Spedag), Dorcas Shikobe (Oserian), Phelistus Kadari (Vihiga Queens), Wincate Kaari (Thika Queens), Elizabeth Ambogo (Spedag), Maureen Khakasa (Trans Nzoia Falcons), Juliet Auma (Thika Queens), Vivian Nasaka (Vihiga Queens)

Viungo: Jentrix Shikangwa (Wiyeta Girls), Mary Kinuthia (Gaspo Youth), Sheril Angachi (Gaspo Youth), Ruth Ingosi (Eldoret Falcons), Corazone Aquino (Vihiga Queens), Elizabeth Wambui (Gaspo Youth), Martha Amunyolete (Trans Nzoia Falcons), Christine Nafula (Gaspo Youth), Cynthia Shilwatso (Vihiga Queens), Mercy Achieng (Thika Queens), Cheris Avilia (Spedag)

Washambuliaji: Neddy Atieno (Makolanders), Esse Akida (Ramat Hasharon), Mwanahalima Adam (Thika Queens), Janet Bundi (Eldoret Falcons), Terry Engesha (Vihiga Queens), Phoebe Oketch (Vihiga Queens), Marjolene Nekesa (USA)

Kenya wapo kundi B pamoja na timu za Taifa za Nigeria, Afrika Kusini na Zambia, na ikumbukwe wamefuzu hatua hiyo baada ya Gini ya Ikweta kufungiwa na Shirikisho la soka Afrika baada ya kuwatumia wachezaji waliozuiliwa.

Sambaza....