Kabla sijakupeleka mbali, kwanza vuta taswira ya paka, kisha mkaribishe kocha wa Simba SC, Patrick Aussem katika medulla ya ubongo wako kisha anza kumtafsiri kwa kukumbuka kama ndiye aliyeirudisha historia iliyoadimika kusikika kwa wekundu wa msimbazi na nchi kwa ujumla baada ya miaka 15 kabla ya kufuzu raundi ya makundi klabu bingwa barani Africa.
Tovuti hii inakuletea mkutano wa kwanza wa kocha wa muda wa Mashetani Wekundi, Manchester United Ole Gunnar na waandishi wa habari uliofanyika jana tarehe 21-12-2018 kufuatia upya wake katika klabu na mechi dhidi ya Cardiff city jumamosi hii.
Klabu ya Real Madrid imethibitisha kuwepo nje kwa takribani wiki nne, sawa na mwezi mmoja kwa mshambuliaji wake, Mhispaniola Marcos Asensio.
Kiungo mjerumani na anayelipwa mshahara mrefu zaidi ndani ya washika mitutu wa London,Arsenal, Mesut Ozil yuko sokoni kwa sasa, na muda wowote huenda akatimkia kusiko julikana.
Miongoni mwa mechi ambazo haziji kusahaulika barani ulaya na duniani kwa ujumla ni mechi ya raundi ya 16 bora klabu bingwa barani ulaya iliyochezwa Machi 8, mwaka 2017 kati ya Barcelona na Paris-Saint Germain. Ilikuwa ni mechi ya marudiano baada ya ile ya kwanza iliyochezwa pale ufaransa na PSG kuibuka na ushindi wa magoli 4-0, katika mchezo huo wa marudiano pale Nou Camp Barca waliibuka na kitita cha magoli 6-1, na kuwasukuma nje ya mashindano PSG.
Baada ya kumtimua kocha wake Jose Mourinho, klabu yaManchester United imemtangaza rasmi mrithi wa mikoba ya mreno huyo Old Traford.
“Usiku wa deni haukawii kuisha” hivi ndivyo kochawa Manchester United Jose Mourinho alivyokuwaakisubilia hatma yake katika klabu hiyo ya mashetani wekundu baada ya matokeomabovu katika ligi na klabu bingwa barani ulaya. Hatimaye imethibitishwa kuwakocha wa mabingwa wa Europa msimu wa 2016/17 ametimuliwa rasmi.
Hivi unamkumbuka Mikel Arteta Amatriain? Achana na Miguel Arteta, mtengeneza filamu, namaanisha yule mkata umeme wa Arsenal miaka ya 2011,aliyekataukame wa vikombe kwa miaka 9 pale kwa washika bunduki wa Arsenal akicheza kama kiungo mkabaji chini yaArsene Wenger.
Katika ulimwengu wa Soka, ukisikia jina la “Jose Mourinho” kuna picha nyingi zinakujia kichwani, napicha hizo zinategemeana na jinsi unavyomkumbuka mreno huyo kwa kile alichoifanyia timu yako au kwa jinsi unavyolijua soka la dunia tangu akiwa Fc Porto na vilabu vingine.
Mpira ni sayansi , yaani lazima kuwe na utaratibu maalumuambao utaiwezesha timu kupata matokeo kutokana na hitaji la mechi husika.