Klabu ya soka ya Asante Kotoko imethibitisha kuingia makubaliano ya miaka mitatu na nahodha wa zamani wa timu ya Taifa ya Ghana Charles Kwablan Akonnor, kuwa kocha mkuu wa timu hiyo Majuma machache baada ya kocha Paa Kwesi Fabin kuachia ngazi na kutajwa kuelekea Afrika Kusini.
Akonnor amekubali kuchukua majukumu hayo baada Majuma mawili ya mazungumzo na viongozi wa klabu ya Asante Kotoko na ameingia kandarasi hiyo jumatatu ya leo mjini Accra.
Akonnor ni kocha huyo wa zamani wa Dreams FC, lakini pia alikuwa akiifundisha timu pinzani ya Asante Kotoko, Ashanti Gold mwaka jana kabla ya kuamua kundoka kutokana na kutokukubaliana kwa baadhi ya mambo.
Aidha hii inakuwa ni timu yake ya tano kufundisha Kocha huyo mwenye umri wa miaka 44, timu nyingine ni Sekondi Eleven Wise, Accra Hearts of Oak, Dreams FC na Ashantigold.