- Safari ya Yanga, Mikononi mwa Dube
- Simba na Yanga nani anaongoza kuweka mpira kwapani.
- Yanga Waweweseka! Gamondi Nje!
- Fadlu Tunaamini anawapa Ubingwa Wekundu
- Manuel Neuer ana umri sawa na uchambuzi wa soka kwa kompyuta
IBRAHIM Ajib ameachwa katika masafara wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ambao umelekea nchini Misri kwa kambi ya mafunzo ya wiki mbili kabla ya kuanza kwa fainali za Mataifa ya Afrika ambazo zinataraji kufanyika nchini humo baadae mwezi huu.
Ajib ambaye aliitwa kwa mara ya kwanza Stars chini ya Mnigeria, Emmanuel Amunike , si Ajib tu hata kiungo mkabaji wa Simba SC, Jonas Mkude nae ameachwa kwa sababu za kimpira lakini nyuma ya hilo wachezaji hao ‘zao’ la timu ya vijana ya Simba wanatakiwa kujirekebesha kiuchezaji hili wapate nafasi.
Timu ya Taifa ni mkusanyiko wa wachezaji bora wan chi katika wakati husika na ukitazama katika miezi hii sita ya mwisho, Ajib amekuwa chini mno kiubora na hili linatokana na namna mchezaji huyo wa mashambulizi alivyoamua kuishi. Amekuwa ‘mtoro’ katika klabu yake, hajitumi na amekuwa mchezaji anmmayecheza kibinafsi mno.
Wakati, Stars ikifuzu kwa fainali zake za kwanza baada ya miaka 39 kupita, Ajib hakuwepo kikosini na mar azote ambazo Amunike alimuacha yalikuwa yakisemwa mengi huku wengine wakidai kuwa mchezaji huyo ameonewa. Kutokujituma, uchezaji wake wa kibinafsi ni sababu kubwa ya kuachwa kwake lakini uwepo wa wachezaji kama Saimon Msuva ni sababu ya Amunike kumpuuza Ajib na kumuondoa kikosini.
Mkude yeye ana matatizo mengi katika uchezaji wake, pasi zake mara nyingi zimekuwa ‘mkaa’, hajali pale anapopoteza mpira, pia kama mchezaji mwenye jukumu la kuunganisha timu na kulinda mchezaji huyo amekuwa akicheza bila nidhamu katika maeneo yake na kwa aina ya wachezaji waliopo kikosi Amunike ameona ni heri amuache kikosini-yupo sahihi.
Kuachwa kwa wachezaji hawa ‘mastaa vijana’ kutoka klabu kubwa nchini za Simba na Yanga kunapaswa kuwafumbua zaidi kimchezo vijana hao kama kweli wanataka kufikia malengo yao makubwa. Ni vijana ambao wana matatatizo mengi nje ya uwanja licha ya vipaji vikubwa walivyonavyo.
Kutokujituma kwao na mchezo usiokuwa na kiwango muendelezo ni sababu kubwa ya kuachwa kwao na wamestahili kuondolewa kikosini kwa sababu Amunike anahitaji kwenda Misri na wachezaji walio timamu kimwili na kiakili- wenye nidhamu ya kimchezo pia. Amunike yupo sahihi kuwaacha wachezaji hawa kutokana na kwamba anahitaji kikosi kinachojitolea na si kulazimishwa kucheza.