Sambaza....

Leo Simba watakuwa mjini Cairo, nchini Misri kutupa karata yao ya tatu katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, ngazi ya makundi. Hizi ni sababu kwa nini Simba anaweza kupoteza dhidi ya Al Alhy.

HALI YA HEWA YA UWANJA WA NYUMBANI.

Mashabiki wa Al Ahly uwanjani kwao.

Moja ya vitu ambavyo timu nyingi za kiarabu hujivunia ni hali yao ya viwanja vya nyumbani. Mara nyingi huwa kuna hali kubwa kuanzia kwa mashabiki mpaka kwa wachezaji.

Mashabiki jukwaani muda mwingi hutumia kuwahamasisha wachezaji wao ndani ya uwanja kuzidi kupigana zaidi. Hali hii inaweza ikawa kikwazo kubwa kwa Simba, kwa sababu mashabiki wa Al Alhly hutengeneza mazingira ya kuwaunga muda wote wachezaji wao ili waweze kufanya vizuri.

MATOKEO MAZURI YA AL AHLY NYUMBANI na MATOKEO MABAYA YA SIMBA UGENINI.

Katika mashindano haya ya ligi ya mabingwa barani Afrika, Al Alhy hajapoteza katika uwanja wao wa nyumbani katika mechi 18 zilizozipita. Wakiwa wameshinda mechi 12 , wakatoka sare michezo 6.

Msemaji maarufu wa Simba Sc, Hadji Manara

Wakati Simba katika mechi 16 zilizopita alizocheza ugenini kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, ameshinda mechi moja, akatoka sare mechi 3 na kufungwa mechi 12.

MATOKEO MABAYA YA SIMBA YA HIVI KARIBUNI.

Baada ya kufungwa goli 5 na As Vita, Simba ilienda kucheza fainali ya kombe la mapinduzi na wakafungwa na Azam FC 2-1.

Baada ya hapo walishiriki mashindano ya Sportpesa Cup na hawakufanikiwa kufanya vizuri walishika nafasi ya tatu.

Kocha wa Simba Sc, Aussems

Kushika kwao nafasi ya tatu siyo jambo ambalo nataka kuliongelea hapa, ila mapokeo ya matokeo haya kwa mashabiki wa Simba yanaweza yakasababisha Simba kushindwa mechi hii.

Mapokeo ya mashabiki wa Simba yalikuwa katika mlango hasi hali ambayo ilisababisha kutokuwa na Amani nzuri tena kwenye klabu hiyo.

Hii inaweza ikawaathiri kisaikolojia wachezaji wa Simba, kwanini nasema hivo ?, Simba wataingia uwanjani wakiwa na presha kubwa ya kupata matokeo ili tu waweze kuwapa imani mashabiki wao.

Andika matokeo ya Al Ahly vs Simba ushinde tiketi ya VIP B.

Kitu hiki kina madhara gani ?, wachezaji wanapokuwa na presha ya kupata matokeo watacheza kwa kukamia, wakicheza kwa kukamia inaweza kuwasababishia wafanye makosa mengi binafsi ndani ya uwanja, makosa ambayo yanaweza yakaifanya timu ifanye vibaya.

SAFU MBOVU YA ULINZI YA SIMBA.

Simba wamekuwa na safu mbovu ya ulinzi kutokana na aina ya kujiuzuia wanayoitumia. Aina ambayo haina wachezaji ambao wanaweza kuicheza.

Wawa, beki wa Simba

Simba inatumia HIGHLINE DEFENSE. Kitu ambacho kinasababisha safu ya ulinzi ya Simba kuwa juu sana kutoka eneo la golikipa.

Kitu hiki huwa kina madhara yapi ?, hii husababisha kuwa rahisi kwa Simba kutengeneza uwazi (space) eneo la nyuma. Uwazi ambao hutumiwa na timu pinzani kuwaadhibu.

Aina hii ya uzuiaji ni nzuri ila inakosa aina ya wachezaji ambao wanaweza kukaba. Kutokana na aina ya wachezaji waliopo kushindwa kuziba spaces ambazo huachwa nyuma.

HISTORIA YA AL ALHLY KWENYE KOMBE HILI.

Al Alhly ndiyo mabingwa wa kihistoria wa kombe hili la ligi ya mabingwa barani Afrika. Kombe hili huwa wanalichukulia kwa maanani sana. Siyo rahisi kwao wao kukubali kupoteza nyumbani tena dhidi ya Simba.

Sambaza....