Mshambuliaji aliyewika katika klabu ya Mwadui FC msimu jana, Salim Aiyee amesaini rasmi kuwa mchezaji wa Kinondoni Municipal Council (KMC FC).
Mchezaji huyo aliyefunga magoli 18 msimu jana kwenye ligi kuu, na akafunga magoli 2 kwenye mechi za mtoano ya kupanda ligi kuu.
Mafanikio hayo yamewavuta KMC FC na kumpa kandarasi la miaka miwili . Changamoto kubwa ambayo atakuwa nayo kwa msimu ujao ni yeye kucheza juu ya mafanikio ya msimu uliopita.