Mara zote katika mashindano yoyote mshindi hupewa tuzo ama kongole, haijalishi itakuwa ndogo ama kubwa ingawa ushindi unaweza kuwa mkubwa au mdogo. Mara zote watu huonyesha uhitaji katika jambo zuri hivyo hulazimika kupigana na kupambana vikali kulipata.
Umoja wa nchi za Afrika Mashariki ( Tanzania, Kenya, na Uganda) umeshinda zabuni ya kuaandaa mashindano ya mataifa Afrika (AFCON) ya mwaka 2027. Mkutano wa wajumbe wa shirikisho la soka Afrika CAF baada ya kukutana tarehe 27 mwezi huu waliwatangaza Morrocco kushinda Zabuni ya kuandaa AFCON ya mwaka 2025 kwa kupigiwa kura 22 ambazo ni asilimia 100% za wajumbe wote na Afrika mashariki (Kenya, Uganda na Tanzania) kwa mwaka 2027.
Afrika Mashariki inapata nafasi ikiwa ndio mara yake ya kwanza katika historia ya mpira wa miguu kupata nafasi hiyo ya kuandaa mashindano makubwa kabisa kwa ngazi ya mataifa Afrika.
Kwa mustakabari huo Tanzania, Kenya na Uganda watalazimika kufanya maboresho makubwa sana katika mambo yafuatayo;
Ujenzi wa viwanja vipya na ukarabati wa vilivyopo.
Serikali pamoja na mashirikisho ya nchi hizi mwenyeji hawana budi kushirikiana katika kuhakikisha viwanja vipya vinajengwa na vile vya zamani vinafanyiwa ukarabati ili kukidhi haja na mahitaji ya mashindano.
Pia ujenzi wa viwanja vya mazoezi unahitajika kwani timu zitaweka kambi na zitahitaji kufanya mazoezi ili kujiwinda bara-bara na mashindano.
Usalama wa misafara na mahoteli.
Usalama humfanya mtu aone yuko huru kufanya jambo, Afrika Mashariki ni ukanda ambao unasifika kuwa na usalama kuliko kanda nyingine zote za Afrika. Lakini hii haitoshi kusema usalama ni mkubwa kuelekea 2027. Usalama katika utunzaji wa miundombinu iliyopo na ile mipya itakayojengwa mfano viwanja na mahoteli ambapo timu zitafikia, lakini misafara ya timu inatakiwa kuwa salama.
Hivyo mashirikisho ya soka ya nchi mwenyeji pamoja na serikali wanatakiwa kuhakikisha usalama na utulivu katika ukanda huu kuanzia sasa mpaka mashindano yatakapoanza na kumalizika kwani suala lolote lisilo la kiusalama likitokea katika kipindi hiki linaweza kutia dosari uteuzi huu na hata kupokonywa nafasi hii.
Licha ya yote nchi wenyeji watakwenda kufadika sana na mashindano haya; kwani upo usemi wa kiafrika usemao “Mgeni njoo mwenyeji ashibe”. Ujio wa mataifa mengine utaacha faida nyingi sana na alama nzuri, nyingi na za kudumu. Faida kadhaa ni kama zifuatazo;
Kukua kwa soka na biashara
Hapa wachezaji wazawa wa nchi wenyeji watapata nafasi kuonekana Duniani kote kwani ulimwengu wote wa soka macho na masikio yao yatakuwa kwao hiyo 2027.
Mashindano haya yataacha mioundombinu mingi na ya viwango ambayo itaruhusu soka kupigwa kwa kiwango cha juu, hivyo baada ya mashindano kumalizika soka litapigwa kwelikweli kwani miundombinu itakuww rafiki.
Kubwa zaidi ni biashara za soka hususani kuuza kununua wachezaji, Timu zetu zitapata nafasi ya kuuza wachezaji na kununua wachezaji. Zaidi ya yote ni biashara za nje ya uwanja zitakuwa kwa kiasi kikubwa mfano biashara za usafiri, vyakula, vinywaji, makazi na hata biashara za jezi. Wafanya biashara watapata na watakuwa na soko la uhakika katika kipindi chote cha mashindano.
Kuutangaza Utalii.
Nchi wenyeji ambao ni Kenya, Uganda na Tanzania wanasifika kuwa na utajiri mkubwa wa vivutio vya utalii kama vile Milima mfano Mlima Kilimanjaro, Mlima Kenya, Lakini uwepo wa mbuga kubwa za wanyama kama vile Mbuga za Serengeti na Masai mara. Mataifa wageni watapata nafasi ya kudhuru maeneo ya kitalii suala ambalo litachagiza kukua kwa utalii na mataifa haya wenyeji kujikusanyia mapato kupitia utalii.
Usisahau Dunia itatazama, Ulimwengu wa Soka utaona vivutio vingi kupitia mashindano haya hivyo tutarajie mafuriko ya watalii wengi.
Kumbuka: DALILI YA MVUA …..?
Jiunge ujadili na Wakandanda wote kwa email yako tu.