
Katika kuelekea mashindano ya kihistoria ya AFCON 2027, Mtandao wako pendwa wa Kandanda.co.tz utakuletea mfululizo wa taarifa mahsusi kuhusu maeneo ya Tanzania yatakayohusika moja kwa moja na mashindano haya makubwa barani Afrika.
Tutakuwa tukikuletea kwa undani:
✅ Viwanja vitakavyotumika – Uwezo, hali ya miundombinu, historia yake, na maandalizi yanayoendelea
✅ Hoteli bora kwa mashabiki na timu – Kuanzia za kifahari hadi za bei nafuu
✅ Mikahawa na Baa maarufu – Chakula, burudani na sehemu za kukutana na mashabiki wengine
✅ Vivutio vya kitalii katika eneo husika – Kwa mashabiki wa nje na wa ndani kutembelea wakati wa mechi
Kupitia mtandao wa Kandanda.co.tz tunaamini ni nafasi nzuri ya kuelimisha na kuwahamasisha mashabiki wa kandanda na watalii kuhusu maandalizi ya AFCON 2027 ambayo ni fahari kubwa kwa Tanzania.