Sambaza....

Shirikisho la kandanda nchini (TFF) limetangaza kuwa Kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” imeanza rasmi jumatatu ya leo kujiandaa na michezo miwili ya kuitafuta tiketi ya kucheza Fainali za Afrika mwakani dhidi ya Cape Verde.

TFF imesema kuwa Kambi hiyo inayoanza leo itaanza na wachezaji wanaocheza katika ligi ya ndani kabla ya kuungana na wale wanaocheza kwenye ligi mbalimbali nje ya Tanzania na kwamba mazoezi yanatarajiwa kuanza kesho asubuhi kwenye Uwanja wa JKM Park, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Maandalizi yatakuwa chini ya Kocha Mkuu Emmanuel Amunike,Wasaidizi Hemed Morocco na Emeka Amadi, huku Madaktari wakiwa ni Dr Richard Yomba na Gilbert Kigadya

Ikumbukwe kuwa Mchezo wa kwanza utachezwa Oktoba 12,2018 kwenye mji wa Praia huko Cape Verde na mchezo wa marudiano utachezwa Oktoba 16,2018 Uwanja wa Taifa ukiwa ni michezo ya kundi L kutafuta Tiketi ya AFCON itakayofanyika mwakani nchini Cameroon.

Kikosi kilichoitwa

Aishi Manula (Simba)

Salum Kimenya(Tz Prisons)

Frank Domayo(Azam FC)

Salum Kihimbwa(Mtibwa),

Kelvin Sabato(Mtibwa)

David Mwantika(Azam FC)

Ally Abdulkarim Mtoni(Lipuli)

Mohamed Abdulrahiman (JKT Tanzania )

Beno Kakolanya (Young Africans)

Hassan Kessy (Nkana,Zambia)

Gadiel Michael (Young Africans)

Abdi Banda (Baroka,Afrika Kusini)

Aggrey Morris (Azam FC)

Andrew Vicent (Young Africans )

Himid Mao (Petrojet,Misri)

Mudathir Yahya (Azam FC)

Simon Msuva (Al Jadida,Morocco)

Rashid Mandawa (BDF,Botswana)

Farid Mussa (Tenerife,Hispania)

Mbwana Samatta (KRC Genk,Belgium)

Thomas Ulimwengu (Al Hilal,Sudan)

Shabani Chilunda (Tenerife,Hispania)

Yahya zaydi(Azam FC)

Kelvin Yondan (Young Africans)

Paul Ngalema (Lipuli)

Jonas Mkude (Simba)

John Boko (Simba)

Shomari Kapombe (Simba)

Feisal Salum (Young Africans)

Abdallah Kheri (Azam FC)

Sambaza....