Sambaza....

Kamati Tendaji ya Shirikisho la Kandanda Barani Afrika (CAF) imeamua kutoivua Ghana uwenyeji wa Michuano ya Mataifa Afrika kwa upande wa Wanawake (AWCON).

Awali taarifa zilisema kuwa Ghana ilipokonywa uwenyeji baada ya kuonekana kusuasua katika kufanya maandalizi, lakini katika kikao cha kamati hiyo kilichofanyika Alhamis nchini Misri, kimeamua kutoa ivua uwenyeji na badala yake kuisaidia kwa Hali na mali ili kufanikisha mashindano hayo.

Timu ya Wanawake ya Nigeria ikishangilia moja ya mechi zao

Aidha kabla ya maamuzi hayo kamati ya muda ya uongozi nchini Ghana iliwasilisha ripoti ya mwisho siku ya Jumatano ikionesha namna walivyojiandaa Kabla ya mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika kuanzia November 17 hadi December 1 Mwaka huu.

Kwa maana hiyo sasa Ghana itaandaa mashindano hayo Kwa mara ya kwanza ambapo tayari Mabingwa mara 9 wa AWCON Nigeria, pamoja na Afrika Kusini, Zambia, Gini ya Ikweta, Mali, Cameroon na Algeria wamefuzu kushiriki mashindano hayo.

Sambaza....