Huku zikiwa zimebaki takribani siku saba pekee kufikia September 30 ambapo Simba na Yanga zitakutana katika mchezo wa ligi kuu Bara tayari joto lá pambano hilo limeshaanza kupanda!
Kwa kuonyesha hilo tayari timu hizo zimeshasogezewa mbele mechi za katikati ya wiki ili zipate muda wa kujianda na mtanange huo. Simba alikua icheze na Biashaara Mara katika uwanja wa karume huku Yanga wao walikua wacheze na JKT Tanzânia uwanja wa Taifa.
Wakati Simba inachukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita ni klabu moja pekee ambayo haukuambulia kipigo kutoka kwa Wekundu wa Msimbazi. Si Yanga wala Azam wala Singida utd bali ni Lipuli fc iliyokua chini ya makocha wachezaji wa zamani wa klabu Simba Selemani Matola na Amri Said.
Katika mchezo wa kwanza Simba ilitoka sare ya bao moja kwa moja jijini Dar es salaam na pia katika mchezo wa raundi ya pili walitoka sare kama hiyo katika dimba la Samora Iringa.
Mwalimu Amri Said msimu huu ameanzaa ligi akiwa na kikosi cha Mbao fc na kuiacha Lipuli chini ya Selemani Matola. Katika mchezo wake na Simba mwalimu Amri aliweza kuiongoza Mbao fc kuilaza bao moja kwa sifuri katika dimba lá Ccm Kirumba Mwanza hivyo kuendeleza ubabe wake dhidi ya makocha wa Simba.
“KWANI SISI NA WAO LINI?”